Katika kikao cha kamati ya ushauri cha Wilaya ya Bunda kilichoongozwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Bunda NduguSalum Khalfani Mtelela siku ya tarehe 6/12/2024 ambaye alikuwa mwenyekiti wa kikao hicho kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mh. Dkt Vicent Anney.
Kikao hicho kilifanyika katika ukumbi wa Malaika uliopo Bunda Mjini na lengo kuu ni kupokea taarifa mbalimbali kutoka katika taasisi zote za Serikali zilizopo katika Wilaya ya Bunda kuzijadili na kuzitolea ufafanuzi kwa wananchi kuhusiana na masuala mbalimbali ya kiuchumi,kielimu,Afya na miundombinu.
Wajumbe katika kikao hicho waliomba na kushauri barabara ya Busambara Mugara iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda,ambayo inaunganisha Wilaya mbili ya Msoma Vijijini na Bunda ambayo ipo chini ya TARURA,kupewa TANROADSili iweze kutengenezwa kwa kiwango cha lami.
Wajumbe walisema sababu ya kuomba barabara hiyo kuchukuliwa na TANROADS ni kwakuwa imekuwa na shughuli nyingi za kiuchumi na kwakuwa inahudumia watu wengi kutoka Wilaya ya Msoma Vijijini na Bunda.
Mwenyekiti wa kikao hicho NduguSalum Khalfani Mtelela aliwauliza wajumbe wote kama wameridhia ombi hilo la kupewa TANROADS kusimamia barabara hiyo na wajumbe wote waliridhia,hivyo walisema ushauri wamechukua na watauwasilisha kwenye kikao cha ushauri cha Mkoa kinachotarajiwa kufanyika siku ya tarehe 12/12/2024 na Mkoa utakaporidhia ombi na shauri hilo, BARABARA hiyo itaanza kuhudumiwa na TANROADS badala ya TARURA.
Ndugu, Mtelelaaliwasukuru wajumbe wote waliohudhuria kikao hicho na alizishukuru taasisi zote zilizo wasilisha taarifa zao na wajumbe kuweza kuzijadili kwa kina.
Kikao cha kamati ya ushauri cha Wilaya ya Bunda kilihudhuliwa na viongozi wa vyama vya siasa,wakuu wa taasisi za Serikali, kamati ya usalama ya Wilaya, viongozi wa dini,wakuu wa divisheni na vitengo kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Mji,Wakurugenzi watendaji wa Halmashauri zote mbili, Wenyeviti wa Halmashauri, Waheshimiwa Madiwani kutoka majimbo yote matatu(Mwibara,Bunda na Bunda Mjini)pamoja na Mbunge wa jimbo la Bunda Mjini, Mh.Roberth Maboto.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda