Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Bi. Changwa M. Mkwazu ambaye ni katibu wa kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango (FUM), alifungua kikao cha robo ya kwanza kwa mwaka 2023/2024 kwa kumkaribisha Mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye ni Diwani wa Kata ya Iramba, Mh. Charles Manumbu siku ya tarehe 3/11/2023, katika ukumbi wa Halmashauri.
Lengo la kikao hicho ni kupokea taarifa mbalimbali za utekelezaji katika kipindi cha robo ya kwanza kuanzia mwezi Julai hadi Septemba, 2023 kutoka katika Idara na Vitengo mbalimbali.
Mwenyekiti wa Kamati, alianza kwa kumpongeza Mkurugenzi Mtendaji kwa hatua aliyochukua kwa kuhamia katika jengo jipya la utawala lililopo Kibara Stoo, ambalo bado ujenzi wake unaendelea, lakini wameweza kuhamia hivyo kwa mujibu wa sheria.
Mh. Manumbu pia, alimuagiza, Mkuu wa Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kuhakikisha kwamba anakusanya mapato ya kutosha kutoka katika vyanzo vyake alivo navyo kwa ngazi zote kuanzia Kata na Vijiji.
Aidha, Mjumbe mmoja wa kamati aliwashauri Waheshimiwa Madiwani kuhakikisha wanasimamia mapato vizuri katika Kata zao kutokana na vyanzo vya mapato vilivyopo.
Pia, aliwaagiza Watumishi kubadilika na kufuata taratibu na sheria za kazi kama zinavyotakiwa, wanapoamua kufanya maamuzi katika mradi wowote ule wahakikishe wanafuata taratibu na sheria za utumishi wa umma.
Kamati ilihitimisha kikao kwa kutoa taarifa ya ziara walioifanya kwa siku mbili katika kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0754335739
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda