Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Ndugu Gerald Kusaya siku ya tarehe 6/03/2025 amefanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi miwili ya elimu inayotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda pamoja na mradi wa ukamilishaji wa jengo la utawala la Halmashauri.
Ziara hiyo ililenga kutembelea na kukagua maendeleo ya miradi pamoja na utekelezaji wa miradi. Aidha, ametembelea miradi ya ujenzi inayoendelea kutekelezwa katika shule ya wasichana Mara (MARA GIRLS) ambapo amekagua ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa, jengo la tehama, makitaba,mabweni manne pamoja na nyumba tatu za walimu na utekelezaji wa miradi hiyo upo katika hatua mbalimbali za ujenzi ikiwemo upauaji kwa baadhi ya majengo, na ufungaji lenta.
Pia, alitembelea na kukagua ukamilishaji wa jengo la utawala la Halmashauri ya Wilaya ya Bunda na ujenzi umefikia asilimia 90 ukiwa katika hatua mbalimbali za ujenzi ikiwemo upakaji rangi na ujenzi wa uzio (fensi).
Ndugu Kusaya alikamilisha ziara yake kwa kutembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa shule mpya ya Sekondari kata ya Nyamihyolo na kukagua jumla ya majengo kumi na tatu na ujenzi umefikia hatua mbalimbali kama upigaji ripu, upauaji,blundering na ufungaji board.
Hata hivyo, Katibu Tawala amepongeza kasi ya utekelezaji wa mradi wa shule mpya ya Nyamihyolo pamoja na jengo la utawala na kusisitiza kuongeza juhudi ili miradi iweze kukamilika kwa wakati. Pia, amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya kufuata utaratibu maalumu wa matumizi ya fedha za uendeshaji wa miradi na kutojihushisha na ulipaji wa madeni ya miradi iliyopita kwa kutumia fedha za uendeshaji wa miradi ya awamu ya pili.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda