Kamati ya siasa ya Wilaya ya Bunda ikiongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi Wilaya ya Bunda Ndugu. Mayaya Abraham siku ya tarehe 10/3/2025 aliongoza wajumbe wa kamati kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda kama ilani ya chama inavyoelekeza kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
Katika ziara hiyo, kamati ilitembelea na kukagua miradi ya ujenzi wa madarasa na mabweni yanayoendelea kujengwa katika shule ya Sekondari ya wasichana Mara, ukamilishaji wa bwalo la chakula, pamoja na ukamilishaji wa bweni Moja la awamu ya kwanza katika ujenzi wa shule ya sekondari ya wasichana ya Mara.
Pia, kamati ilitembelea na kukagua maendeleo ya ukamilishaji wa shule ya Sekondari Mayolo inayoendelea kujengwa huku, ujenzi ukiwa katika hatua mbalimbali za ukamilishaji, wajumbe wa Kamati walipongeza na kuridhishwa na ujenzi mzima unavyoendelea.
Wajumbe pia, walitembelea na kukagua chuo cha ufundi Veta, shule ya Sekondari ya Amali iliyopo Makwa, kituo cha Afya Isanju, mradi wa maji Karukekere na pia walitembelea na kukagua barabara ya Busambara Mugara na ukamilishaji wa vyumba vitatu vya madarasa na matundu sita ya vyoo katika shule ya msingi Namibu A.
Katika shule ya msingi Namibu Mwenyekiti wa kamati ya siasa, alimuagiza Katibu Tawala wa Wilaya ya Bunda kuhakikisha vyumba vitatu vya madarasa kutokutumika kutokana na uchakavu wa miundo mbinu yake, hivyo aliagiza ukamilishaji wa vyumba vitatu vilivyopo shule ya msingi Namibu A vikamilike kwa wakati ili wanafunzi waweze kutumia vyumba hivyo.
Wajumbe wa Kamati ya siasa walipongeza na kuridhishwa na usimamizi mzuri wa miradi ya ujenzi wa maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.
Kamati ilihitimisha ziara yake kwa kufanya kikao na wananchi wa Kijiji cha Sikiro, ambapo Mwenyekiti wa Chama alimuagiza katibu Tawala wa Wilaya ya Bunda kuhakikisha anafanya kikao na wanakijiji ili kuweza kujenga mahusiano mazuri kwa ajili ya kudumisha amani ya Kijiji na kukuza uchumi wao.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda