Kamati ya siasa Wilaya ikiongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi Wilaya ya Bunda Ndugu. Mayaya Abraham, siku ya tarehe 18/03/2025 wamefanya kikao cha majumuhisho ya ziara iliyofanyika katika majimbo matatu yaliyopo Wilaya ya Bunda.
Akifungua kikao hicho Ndugu. Mayaya amesema kamati ya siasa imekuwa na utaratibu wa kutembelea na kukagua maendeleo ya miradi inayotekelezwa katika majimbo yote matatu, ambayo ni jimbo la Mwibara, Jimbo la Bunda Mji na Jimbo la Bunda.
Katika kikao hicho kamati iliwasilisha taarifa ya ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo katika Wilaya ya Bunda na kutoa maelekezo ya jumla katika utekelezaji wa miradi hiyo.
Aidha, Ndugu Mayaya amewataka wakuu wote wa Idara na vitengo kushirikiana na Mkuu wa Wilaya katika kutekeleza majukumu yao ili kurahisisha utendaji kazi na kepuka sitofahamu zisizo za lazima katika Wilaya ya Bunda.
“Sisi kama chama tutashirikiana na Mkuu wa Wilaya pamoja na watumishi wote ili kuhakikisha tunawekana sawa” Amesema Mayaya
Kwa upande wake Mkuu wa Wialaya ya Bunda Mh. Aswege Enock Kaminyoge, ameahidi kutekeleza na kufuata maelekezo yote yaliyotolewa na kamati ya siasa, na kuishukuru kamati hiyo kwa utendaji kazi mzuri na umahiri wa kufuatilia na kukagua miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa katika wilaya ya Bunda.
Pia, amezishauri kamati za fedha za Halmashauri zote mbili kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia kanuni na taratibu pasipo ubaguzi, upendeleo na hofu.
Hatahivyo kikao hicho kilihudhuriwa na Kamati ya siasa,Mkuu wa Wilaya ya Bunda,Katibu tawala wa Wilaya ya Bunda pamoja na wakuu wa vitengo wa Halmashauri na Wakuu wa taasisi za serikali.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda