Mwenyekiti wa Kamati ya siasa Wilaya ya Bunda, Ndugu. Mayaya Abrahamu siku ya tarehe 12/3/2025 ameongoza wajumbe wa Kamati katika ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
Katika ziara hiyo, wajumbe walitembelea na kukagua ukamilishaji wa zahanati ya Tiringa'ati, ambapo wajumbe walipongeza na kuridhishwa namna mradi huo unavyoendelea ambapo, mwenyekiti aliagiza kasi iongezwe katika ukamilishaji ili zahanati iweze kufunguliwa na ianze kutoa huduma mapema mwezi wa nne.
Wajumbe wa kamati walitembelea na kukagua miradi ya maji ya Nyamuswa na Mugeta, ujenzi wa barabara ya Mekomariro, nyumba ya watumishi katika shule ya sekondari Mariwanda, ukamilishaji wa ujenzi wa shule ya Sekondari Nyaburundu, ujenzi wa zahanati ya Mahanga, ambapo ipo katika hatua za upauaji, pia, walitembelea na kukagua maendeleo ya ufyatuaji wa matofali kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya Madarasa katika shule ya msingi Mugeta na nyumba ya Mwalimu Nyang,alanga.
Wajumbe wa Kamati ya siasa waliiridhishwa na miradi yote ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa na pia waliwapongeza viongozi wote wa taasisi na Halmashauri kwa namna wanavyoisimamia miradi hiyo vizuri katika utekelezaji wake.
Aidha, katika ziara hiyo Mwenyekiti pamoja na wajumbe wa Kamati, walitembelea mradi wa ujenzi wa shule ya msingi Nyansirori, na Mwenyekiti wa Kamati alimuagiza Katibu Tawala wa Wilaya kuhakikisha anawatuma Taasisi ya Kupambana na kuzia rushwa (TAKUKURU) kuchunguza mwenendo mzima wa mradi unavyoendelea, hii ni kutokana na na changamoto chache walizozibaini katika mradi huo.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda