Kupitia mradi wa kuhimili mabadiliko ya Tabianchi (BCRAP), Halmashauri ya Wilaya ya Bunda siku ya tarehe 17/12/2023 ilipokea vifaranga vya kuku zadi ya 700, pamoja na mifuko ya chakula cha kuku zaidi ya 70 yenye ujazo wa kilo 50 kila mfuko.
Mratibu wa mradi wa kuhimili mabadiliko ya Tabianchi, Ndugu Johannes Bucha, alisema vifaranga hivo, pamoja na chakula vitasambazwa kwenye vikundi 8 vilivyopo katika Kata ya Neruma na Namhula ambavyo vilishapewa mafunzo ya namna ya utunzaji wa vifaranga hivyo.
Naye Diwani Kata ya Neruma, Mh. Fortunatus Maiga alimshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, Bi. Changwa M. Mkwazu kwa mapokezi mazuri ya vifaranga hivo ambapo aliahidi kuwasimamia wananchi wake katika kuhakikisha mradi huo wa ufugaji wa vifaranga huo unaenda vizuri na unafikia lengo tarajiwa.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda