Halmashauri ya Wilaya ya Bunda imeadhimisha siku ya UKIMWI duniani kwa kufanya shughuli mbalimbali katika maadhimisho hayo ambapo walizindua kampeni ya utoaji wa matone ya Vitamin A kwa watoto wenye umri wa miezi sita hadi 59, utoaji wa dawa za minyoo kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano, uchangiaji wa damu, upimaji wa malaria, na homa ya ini.
Maadhimisho hayo yalifanyika siku ya tarehe 1/12/2024 katika stendi ya mabasi Nyamuswa na mgeni rasmi alikuwa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Mh. Keremba Irobi.
Mh. Irobi alisema Halmashauri ya Wilaya ya Bunda imeendelea kutekeleza shughuli mbalimbali zinazohusiana na upimaji wa virus vya UKIMWI kwa kufanya upimaji wa Mara kwa mara kuanzia ngazi za vituo vya Afya, Zahanati na kwenye hospitali ya Wilaya.
Hali ya maambukizi katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda imeshuka hadi kufikia asilimia 2.1 ambapo inaonyesha jamii imeanza kuelimika na kuhamasika kwenda kupima mara kwa mara kwa lengo la kujikinga na maambukizi mapya ya virus kwa kuhakikisha wanaanchana na Mila potofu za kurithi wajane na wagane, kufanya tohara kwa njia za kienyeji kwani zimekuwa kichocheo kikubwa cha kuongezeka kwa Virus vya UKIMWI.
" Leo hii inaonyesha ni kwa jinsi gani maambukizi ya virus vya UKIMWI yanavoshuka, hivyo inaonyesha ni kwa jinsi gani jamii inavyoanza kujali katika kuhakikisha inadhibiti maambukizi ya virus vya UKIMWI." Alisema Mh. Irobi.
Lengo kuu la maadhimisho haya ni kutafakari hali halisi ya mwelekeo wa kudhibiti maambukizi ya virus vya UKIMWI kitaifa na kimataifa. UKIMWI umekuwepo nchini Tanzania kwa zaidi ya miaka 40 sasa na unaendelea kuleta athari kubwa katika jamii kiuchumi na kijamii katika Taifa letu, hivyo hatuna budi kuachana na Mila potofu.
Maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani yalihudhuriwa na wadau kutoka Amref, na USAID kizazi hodari.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda