Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Mheshimiwa Lydia Bupilipiliamepokea taarifa ya utekelezaji wa chanjo ya SuruaRubella na Polio yaSindano kutoka kwa Kamati ya Afya ya Msingi (PHC) Novemba Mosi mwaka huu katikaUkumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya.
Kampeni yachanjo hizo ilianza Oktoba 17 na kumalizika Oktoba 21, mwaka huu ambapowalengwa wa chanjo hizo walikuwa ni watoto chini ya miaka mitano.
Idadi yawatoto waliolengwa kupata chanjo ya Surua Rubella ilikuwa 50,036 kutokana idadikuongezeka watoto 51,036 walipata chanjo ambapo ni sawa na asilimia 102.
Kwa upandewa Polio Sindano walengwa ni watoto wa kuanzia mwaka mmoja na nusu hadimiaka mitatu na nusu.
Idadi yawaliolengwa kupata chanjo ya polio Sindano ni 19,869 kutoka na na idadikuongezeka watoto 22,822 walipata huduma ni sawa na asilimia 115.
Wanakamati yaAfya ya Msingi, wameeleza baadhi ya changamoto walizokutana nazo wakati wakampeni ya chanjo hizo kuwa ni mvua ambapo baadhi ya wazazi walishindwakupeleka watoto vituoni kwa wakati, pia mwitikio na uhamasishaji mdogo katika kata ya Kibara.
Kutokana na haki hiyo, Mheshimiwa Bupilipili ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamatiya Afya ya Msingi, alisema ili kuboresha huduma na kupata mwitikio wa wananchi ni kuandaa chakula bora kwa ajili ya mtoto ambacho kinapatikanakatika jamii.
Alisemakamati inaweza kuandaa hata uji ili wakati mtoto anachomwa sindano anapatakikombe cha uji.
Alitoamsisitizo kwa wanakamati kuwa wabunifu huku akimwagiza afisa Lishe, JanuaryDalushi kusimamia suala la lishe pindi zoezi hilo litapoanza tena.
Kwa upandemwengine Mh Bupilipili alitolea mkazo suala la vifo vya wajawazito na watotokucheleweshwa kwenda kliniki lisije likatokea tena katika Wilaya ya Bunda.
Mwishoaliwapongeza kwa kazi nzuri na kuwataka waendelee kuwajibika katikamajukumu yao kwa ufasaha.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda