Baraza la madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Bunda siku ya tarehe 20/02/2025 katika mkutano wake maalumu uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri limeridhia na kupitisha rasimu ya bajeti ya Tsh.36,516,498.215 kwa mwaka wafedha 2025/2026.
Akisoma bajeti hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Mkuu wa Idara ya mipango na Uratibu Ndugu. Gervas Amata ametoa mchanganuo wa bajeti hiyo ambapo kiasi cha Tsh. Billion 2,650,740,00.00 ni kwa ajili ya mapato ya ndani, Tsh 22,484,500,000.0 kwa ajili ya ruzuku ya mishahara ya watumishi, Tsh. 2,230,254,000.00 kwaajili ya ruzuku ya matumizi mengine na Tsh.9,151,274,215.00 kwaajili ya miradi ya maendeleo.
Akizungumza katika baraza hilo Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Mh. Keremba Irobi, amelipongeza baraza la madiwani kwa kupitisha rasimu ya bajeti hiyo kwani imezingatia mapendekezo yote muhimu ya waheshimiwa madiwani na hivyo itakwenda kutatua changamoto mbalimbali za wananchi.
Kwa upande wake katibu Tawala wa Wilaya ya Bunda Ndug. Salum Khalfani Mtelela ameipongeza Halmashauri kwa ukusanyaji mzuri wa mapato ya ndani na kuwasihi kusimamia bajeti hiyo pindi itakapopitishwa.
“Kupitisha bajeti ni jambo moja lakini pia kuisimamia bajeti hiyo ni jambo lingine hivyo niwaombe mara baada ya bajeti hii kupitishwa na kupokea fedha kwa mwaka 2025/2026 zingatieni vipaumbele na timizeni malengo ya bajeti hii.” Alisema Ndugu. Mtelela
Hata hivyo, miongoni mwa vipaumbele vya Halmashauri katika mpango na bajeti ya 2025/2026 ni kukitangaza kisiwa cha Rwiga kwaajili ya shughuli za utalii, na ulipaji wa madeni ya wazabuni katika Halmashauri.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda