Halmashauri ya Wilaya ya Bunda imepokea fedha kiasi cha Shilingi Bilioni Moja kwaajili ya ujenzi wa makao Makuu ya Halmashauri.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Bw.Stafa Nashoni katika Kikao cha Baraza la Madiwani robo ya pili kilichofanyika Aprili 1, 2021 katika ukumbi wa Kanisa la Kibara.
Bwa.Nashoni alisema kuwa takribani wiki tatu zilizopita Halmashauri ilipokea fedha kiasi cha shilingi Bilioni Moja kwaajili ya ujenzi wa Makao Maku ya Halmashauri.
‘Tunaishukuru Serikali kwakutupatia fedha kwaajili ya Ujenzi”.Alisema Bwa.Nashoni
Hata hivyo Bwa. Nashoni aliwaomba Waheshimiwa madiwani kuacha malumbano ya wapi Halmashauri hiyo ijengwe na badala yake wajielekeze kwenye ujenzi ili uweze kukamilika kwa wakati.
‘Niwaombe waheshimiwa Madiwani tujielekeze katika ujenzi,hatutapenda tena kuoneshewa vidole kila siku tuko nyuma kama ilivyo katika Hospitali’.Alisema Bwa.Nashoni
Mchakato wa Ujenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda ulianza tarehe 30/12/2019 mpaka 18/02/2021 baada ya kupokea Barua ya Katibu Mkuu Tamisemi ikielekeza Maamuzi ya Madiwani yazingatiwe kuwa ujenzi wa Makao Makuu ufanyike Kibara,Kijiji cha Kibara stoo Tarafa ya Nansimo.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda