Balozi wa Sweden nchini Tanzania Bi. Charlota Marcias ameupongeza mkoa wa Mara kwa kutumia ipaswavyo fedha za mradi wa Elimu wa Global Partnership for Education (GPE LANES) kwa kujenga miundombinu ya Shule ambayo imesaidia kupunguza changamoto ya msongamano wa wanafunzi madarasani.
Hayo ameyasema tarehe 22/11/2024 alipokuwa akifanya ukaguzi wa mradi huo wa Elimu katika Shule ya msingi Ibwagalilo iliyopo kata ya Chitengule katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.
Amesema kuwa lengo la kutembelea mradi huo wa Elimu ni kuona kama ushirikiano waliyo nao na Serikali ya Tanzania unafanyika kama wanavyo tarajia na kuongeza kuwa ameridhishwa na utekelezaji wa mradi huo katika mikoa aliyo pita kutembelea na kukagua miradi hiyo.
"Tumeanzia Mkoa wa Arusha, Ngorongoro na hatimaye mkoa wa Mara lengo la kuanzisha mradi huu ni kuimarisha ushirikiano na kukuza sekta ya Elimu nchini Tanzania "Amesema Bi. Marcias
Kwa upande wake Naibu katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Dkt.Charles Mahera amewahimiza viongozi waliopo Wilayani na Mikoani kuimarisha usimamizi pindi wanapo pata pesa za ufadhili kwa ajili ya kuboresha miundo mbinu ya Elimu ya Tanzania.
" Ili Elimu iwe bora na wanafunzi wapate ujuzi na maarifa yatakayo wasaidia ni lazima kuboresha kwanza miundo mbinu ya Elimu na Serikali inapambana sana ili kuhakikisha inaboresha miundombinu ya Elimu kwahiyo lengo la ukaguzi huu ni kujiridhisha kama kweli pesa za mradi wa GPE zimetumika kama zilivyo pangwa"Amesema Dkt. Mahera
Naye, Mkurugenzi Msaidizi anayesimamia Elimu ya Awali na Msingi Suzan Nyambula amesema utekelezaji wa mradi unaridhisha kuanzia thamani ya fedha, ubora pamoja na Ushiriki na wawekezaji wa mradi huo wameridhika kabisa na utekelezaji wa mradi huo kwa maeneo yote waliyopita na kwa sasa wanafunzi wamepunguza utoro wa kuhudhuria shuleni.
Hata hivyo, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Ibwagalilo Isack John amesema uwepo wa mradi huo umesaidia kupokea wanafunzi kutoka maeneo mbalimbali na kuongeza kuwa uwepo wa ufadhili huo umeleta matokeo Mazuri kwa wanafunzi wa darasa la nne kwa mwaka wa masomo 2023/2024 ambao katika mitihani yao ya jipime darasa la nne wote walifaulu.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda