Katibu Tawala Mkoa wa Mara Ndugu Msalika Makungu alitembelea na kukagua miradi mbalimbali ya ujenzi inayoendelea katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda siku ya tarehe 12/10/2023.
Katibu Tawala alisema, Serikali ina sera ya kuanzisha Zahanati kwa kila Kata katika Halmashauri zote nchini na ndio maana wamekuwa wakitoa fedha kwa kila Kata kuhakikisha ujenzi wa Zahanati unakamilika kwa wakati na Wananchi wanapata huduma zilizo bora.
Katibu Tawala Mkoa, akikagua Hospitali ya Wilaya iliyopo katika Kata ya Nyamuswa, Kijiji cha Bukama.
“Lakini kitu cha muhimu tunachoangalia ni wingi wa wahitaji wa huduma hiyo, maana unaweza peleka sehemu huduma ya kituo cha Afya wakati hakuna uhitaji katika eneo hilo, hivyo alimshauri Mkurugenzi Mtendaji kabla hawajaanzisha mradi wowote katika Kata ama Kijiji kwanza waangalie na wingi wa wahitaji katika eneo hilo na sio kuanzisha miradi ambao mwisho wake ni hasara kwa serikali na kuongeza majengo yasiyohitajika”. Alisema Ndugu Makungu.
Katibu Tawala Mkoa, akikagua maendeleo ya Ujenzi wa Shule ya Mkoa ya Wasichana iliyopo katika Kijiji cha Bulama, Kata ya Butimba.
Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Bi. Changwa M. Mkwazu alimwambia Katibu Tawala katika Zahanati alizotembelea na kukuta bado kidogo ukamilishaji wake, Halmashauri imewawezesha sehemu ya mapato ya ndani kuhakikisha wanazikamilisha kwa wakati, hadi mwisho wa mwezi wa Kumi zote ziwe zimeshaanza kutoa huduma kwa Jamii.
Zahanati ya Ragata
Katibu Tawala Mkoa, akikagua Zahanati ya Ragata ambayo ipo katika hatua za ukamilishaji.
Miradi aliyotembelea ni pamoja na Hospitali ya Wilaya iliyopo Nyamuswa katika Kijiji cha Bukama, Zahanati ya Kyandege, Ujenzi wa Shule ya Mkoa ya Wasichana iliyopo katika Kijiji cha Bulamba, Kata ya Butimba, Zahanati ya Ragata, Shule mpya ya Sekondari ya Ragata iliyopo Kata ya Kasuguti, Zahanati ya Neruma iliyopo Kijiji cha Neruma, Kata ya Neruma na Jengo jipya la Utawala la Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda