• Malalamiko |
    • Maswali |
    • Barua Pepe |
Bunda District Council
Bunda District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Kilimo, Umwagiliaji & Ushirika
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji
      • Fedha & Biashara
      • Ujenzi
      • Afya
      • Mifugo & Uvuvi
      • Elimu Sekondari
      • Rasilimali Watu
      • Maendeleo ya Jamii
      • Usafi & Mazingira
      • Elimu Msingi
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ufugaji Nyuki
      • Uchaguzi
      • Manunuzi
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Elimu Msingi
    • Barabara
    • Mifugo
    • Afya
    • Mazao ya kilimo
  • Fursa za Uwekezaji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha, Uongozi & Mipango
      • Elimu, Afya & Maji
      • AIDS Control
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Uma
    • Video
    • Hifadhi ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Ziara ya kamati ya fedha,Uongozi na Mipango katika maeneo ya vyanzo vya mapato Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.

Posted on: November 12th, 2021

Kamati  ya Fedha  Uongozi  na Mipango  Halmashauri  ya Wilaya  ya Bunda  imefanya ziara katika  Josho  la sarakwa na katika vyanzo vya mapato vya Halmashauri Novemba 10 hadi 11,2021.

Akiwasilisha taarifa fupi ya ujenzi wa Josho  Mtendaji wa Kijiji cha Sarakwa Bwa. Shedrack Ezra alisema kuwa ujenzi huo umeanza  22.07.2021 na mpaka kukamilika kwa Josho hilo  itagharimu kiasi cha Tsh,23,481,000.

Bwa. Ezra  alibainisha chanzo cha fedha za ujenzi wa Josho hilo ni Wizara ya Uvuvi na Mifugo  imetoa Tsh. 18,000,000 na  Tshs.5,481,000 nguvu za wananchi wa Sarakwa.

‘Josho hili limeanza kujengwa 22.07.2021 na Inategemea kumalizika mwishoni mwa Mwezi Novemba, 2021’’Alisema Bwa.Ezra

Aidha bwa.Ezra aliongeza kusema  kuwa ujenzi wa josho unaendelea kutekelezwa kwa kuzingatia sheria na taratibu zote  za ujenzi,viwango stahiki vya ubora, na usalama wa mifugo.

Wakizungumza mara baada ya kupokea taarifa fupi na kukagua josho ,wajumbe wa kamati waliridhishwa na mwenendo wa ujenzi wa josho hilo na kushauri kuwa mara nyingine wanapoandika andiko kwaajilii ya mradi wahakikishe kuwa mahitaji yote yanakuwepo katika andiko,kwani imebainika kuwa kuna gharama za ujenzi wa kisima kirefu kwaajili ya maji hazikuwepo katika maombi ya awali.

‘Ujenzi unaridhisha,niwapongeze Wananchi wa sarakwa kwakuendelea kujitolea katika shughuli za maendeleo’’alisema Mhe.Irobi

kamati pia ilitembea Machimbo  yaliopo  kijiji cha Nyaburundu  kata ya Ketare ambapo ilipokea taarifa kutoka kwa kiongozi wa wachimbaji Madini  Bwa. Steve Mwita   kuwa Mgodi hauzalishi kutokana na mashimo kujaa maji.

Bwa.Mwita ameiomba serikali kuwawekea umeme katika  eneo hilo ili uchimbaji  uwendelee,kwani kwasasa wanatumia gharama kubwa  katika  kutoa maji  kutokana  hakuna umeme

"Gharama inayotumika kwasasa ni kubwa kutoa maji katika mashimo,kutokana mashine inatumia mafuta na haina nguvu ya kutoa maji ,hivyo tunaomba  tuletewe umeme  tufanye kazi na kuleta mapato Halmashauri "alisema Bwa.Mwita

Maeneo mengine yaliyotembelewa na kamati ni Mwalo wa Mugara,Isanju, Mugara Nyalina,Muranda na Sikiro ambapo kamati ilibaini kuwa baadhi wa wakusanyaji mapato wamekuwa si waaminifu kwakukaa na fedha muda mrefu bila kupeleka benki  na  wakati mwengine  kutumia fedha mbichi.

Aidha kamati  ilitoa agizo kwa wakusanya ushuru  wote  kuweka fedha zote walizonazo katika akaunti kufikia 19,November 2021.

Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI KWA NAFASI ZA UDEREVA May 07, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO September 26, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI September 18, 2024
  • TANGAZO KWA WATUMISHI WOTE December 20, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU VYATEMBELEWA NA KUKAGULIWA NA KAMATI YA MIKOPO NGAZI YA HALMASHAURI

    April 26, 2025
  • WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA BUNDA WAHITIMISHA MAFUNZO YA SIKU 5 YA UANDAAJI NA UTENGENEZAJI WA MPANGO MKAKATI

    April 25, 2025
  • PROJECT ZAWADI YAIPIGA TAFU MASHINDANO YA UMITASHUMTA KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA BUNDA

    April 07, 2025
  • WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA BUNDA WAPEWA TUZO NA ZAWADI .

    April 03, 2025
  • Angalia zote

Video

Mvamizi wa eneo la soko.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Baraza la Madiwani
  • Dira na Dhamira
  • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Mpango Mkakati
  • Mpango wa Uwekezaji Sekta ya Samaki
  • Muundo wa Taasisi
  • OPRAS - Form

Viunganishi Muambata

  • Matokeo ya Darasa la Saba 2023 Bundadc
  • Matokeo ya darasa la saba
  • Matokeo ya darasa la saba
  • PO-RALG
  • PO-PSM
  • Matokeo ya Kidato cha Nne 2019

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Kibara Stoo.

    Anuani ya Posta: 126, Bunda

    Simu: 0282621055

    Hamishika: 0742163056

    Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda