Wiki ya Elimu kwa Mwaka 2017 imeadhimishwa Mkoani Mara katika Wilaya ya Bunda ambapo Wanafunzi toka Halmashauri zote 9 za Mkoa wa Mara walijumuika pamoja katika kuadhimisha siku hiyo. Wanafunzi hao waliambatana na Viongozi mbalimbali toka katika halmashauri zao ikiwa ni pamoja na Wakurugenzi Watendaji, Maafisa Elimu na Wadua mbali mbali wa Elimu katika halmashauri hizo. Pia, timu ya uratibu toka ngazi ya mkoa ilishiriki kikamilifu ikiongozwa na Afisa Elimu Mkoa wa Mara. Jumbe mbalimbali toka kwa Wanafunzi hao ziliwasilishwa kupitia Ngonjera, Nyimbo, Mashairi, nk na kupokelewa na Mgeni rasmi na wadau mbalimbali wa Elimu kwa ajili ya kufanyiwa kazi.
Kaulimbiu ya maadhimisho hayo ilikuwa ni "Inua Stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu, Jenga Uchumi wa Kati Mkoa wa Mara" ambapo kauli mbiu hiyo ilikuwa inaunga mkono juhudi za Rais katika kuhakikisha kuwa Taifa linakuwa na Wasomi watakaosaidia Taifa kufikia uchumi wa Kati.
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara Dr. Charles Mlingwa ambaye kutokana na kubanwa na majukumu mengine aliwakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Bunda Ndg. Lidya Bupilipili. Pamoja na mambo mengine, hotuba ya Mgeni rasmi ilisisitiza juu ya Walimu kujituma zaidi katika kuwasaidia Wanafunzi wao kielimu na Wanafunzi pia kutakiwa kujifunza kwa bidii ili kufikia malengo ya kitaifa ya elimu bora kwa wote. Wazazi nao hawakuachwa nyuma katika kuhakikisha kuwa wanawapeleka watoto wao shule, kuwasimamia na kuhakikisha kuwa muda mwingi unatumiwa shuleni badala ya kufanya shughuli za nyumbani na hivyo kuwanyima watoto muda na ari ya kuzingatia masomo shuleni.
Maadhimisho hayo pia yalihusisha Wadau muhimu wa Elimu mkoani Mara ambao ni pamoja na PCI, Right to Play, nk.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda