Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndg. Kassim Majaliwa Majaliwa amefanya ziara Wilayani Bunda ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kikazi Mkoani Mara. Ndg. Majaliwa alipokelewa na Viongozi mbalimbali wa Wilaya ikiwa ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Bunda Ndg. Lydia Bupilipili, Katibu Tawala (W) Ndg. Masalu Kisasila, Wenyeviti wa halmashauri za Mji na Wilaya, Wakurugenzi wote 2 wa Halmashauri za Mji na Wilaya, Viongozi wa Vyama vya Siasa na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama wilayani hapa.
Pamoja na mambo mengine Waziri Mkuu aliweza kuzindua miradi ya Wodi ya Wazazi Hunyari, Mradi wa umwagiliaji Kisangwa na Shamba darasa la Mkoa wa Mara lililo wilayani Bunda kama shamba la mfano la kilimo cha pamba. Pia, Waziri Mkuu alifanya mkutano wa hadhara katika uwanja wa sabasaba ambapo alipata fursa ya kuongea na wananchi ikiwa ni pamoja na kusikiliza kero zao na kuzipatia ufumbuzi.
Kero kuu iliyojitokeza ambayo Waziri Mkuu alitoa maagizo yaliyolenga kupunguza ama kuiondoa kabisa ni tatizo la muda mrefu la ukosefu wa maji safi, alama na ya kutosha wilayani hapa.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda