Watumishi wa halmashauri ya Wilaya ya Bunda wamashiriki katika siku ya mazoezi ya viungo kitaifa iliyofanyika tarehe 9/12/2017. Ushiriki huu ni utekelezaji wa maagizo ya ya kitaifa yaliyotolewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu.
Mazoezi hayo yamefanyika katika uwanja wa sabasaba uliopo eneo la Bunda Mjini. Mazoezi hayo pia yaliwahusisha wananchi wengi waliojitokeza kushiriki katika shughuli hii muhimu kwa mustakabali wa afya zao katika kujiepusha na magonjwa yasiyoambukizwa.
Mazoezi haya pia yamefanyika kama sehemu ya maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Taifa letu ambayo uadhimishwa kila siku ya tarehe 9 mwezi wa 12. Akiongea na washiriki wa mazoezi na maadhimisho hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Bwana Amosy Kusaja amewahimiza watumishi na wananchi wote kwa ujumla kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika kutekeleza maagizo mbalimbali yanayotolewa na viongozi wa kitaifa ikiwa ni pamoja na kushiriki katika siku ya usafi kitaifa ambayo hufanyika kila jumamosi ya mwisho ya kila mwezi. Pia aliwataka wananchi wote kuhakikisha wanatambu na kuzienzi harakati za Hayati Baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika kupigania Uhuru wan chi yetu uliopatikana kwa njia ya amani bila ya kumwaga damu mnamo tarehe 9/12/1961.
Akihitimisha siku hii ya mazoezi na maadhimisho ya siku ya Uhuru wa nchi yetu, mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Bunda Bwana Josephat Wambura aliwahimiza wananchi wote wenye umri wa kuanzia miaka 18 kuhakikisha wanashiriki katika zoezi la utoaji wa vitambulisho vya kitaifa linaloendelea kwa sasa katika Wilaya ya Bunda.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda