Afisa ustawi wa jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Bi.Maria John amewataka watu wenye ulemavu katika kata ya Nyamanguta, Ketare na Kata ya Nyamuswa kuunda vikundi ili waweze kupata mikopo inayotolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Bunda itakayowasaidia kujikwamua kiuchumi.
Ameyasema hayo katika ziara ya kuwatembelea watu wenye ulemavu ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Bunda iliyofanyika siku ya tarehe 7/11/2024 huku lengo kuu likiwa ni kutoa Elimu ya kupinga ukatili wa kijinsia kwa watu walemavu na kubaini changamoto inayopelekea watu wenye ulemavu kushindwa kujitokeza kuomba mikopo hiyo.
Hata hivyo amesema kuwa mikopo inayotolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Bunda imegawanyika katika makundi matatu ambayo ni kundi la wanawake, kundi la vijana pamoja na kundi la watu wenye ulemavu, lakini mpaka sasa kundi la watu wenye Ulemavu hawajajitokeza kuomba mikopo hiyo.
"Mwisho wa maombi ya mikopo kwa robo ya kwanza ili kuwa tarehe 31/10/2024 lakini watu wenye ulemavu hawajajitokeza kuomba mikopo hiyo na pesa zenu zipo, sasa tunatamani tufahamu shida ni nini hasa au hamuhitaji mikopo hiyo,na niwakumbushe tu kuwa mkichukua mkopo itawasaidi kujikwamua kiuchumi na kuepuka kuwa tegemezi"Amesema Afisa ustawi wa jamii
Kwa upande wake Afisa Maendeleoya Jamii Ndugu Justin Mtopwa ametoa Elimu ya namna sahihi ya kuomba mikopo hiyo na sifa zinazohitajika kwa waombaji wa mikopo hiyo,huku akiwasisitiza watu wenye ulemavu kujitokeza kuomba mikopo kwani itawasaidia kuinua uchumi wa vikundi na mtu mmoja mmoja.
Mwenyekiti wa Chama cha Watu wenye UlemavuTanzania katika Halmashauri Wilaya ya Bunda Ndugu Sabasaba Mseveni Haji amewahimiza watu wenye ulemavu kujitokeza kushiriki uchaguzi wa vyama vya watu wenye Ulemavu utakao fanyika tarehe 15 mwezi huu 2024 ili waweze kuchagua viongozi sahihi watakao tetea haki za watu wenye Ulemavu.
"Tunashindwa kupata haki zetu kwa sababu hatuna viongozi wanao tutetea hivyo niwaombe kujitokeza kushiriki uchaguzi wa vyama vya walemavu lakini pia tujitokeze kugombea na kupiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 ili tupate wawakilishi sahihi watakao tusimamia vyema" Amesema Sabasaba
Hata hivyo uchaguzi wa vyama vya watu wenye Ulemavu utafanyika katika ngazi ya Halmashauri na Wilaya na utawahusisha watu wenye ulemavu wa Viungo peke yao.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda