Hospitali Mpya ya Wilaya ya Bunda Mkoani Mara iliyojengwa katika kijiji cha Bukama,Kitongoji cha Misheni Kata ya Nyamswa imeanza rasmi kutoa huduma kwa Wananchi wa Halmashauri hiyo baada ya kukamilika kwa ujenzi wa miundombinu kwa awamu ya kwanza ambapo Zaidi ya bilioni 1.5 zilitumika na kiasi cha shilingi milioni 300 zimetolewa kwa awamu ya pili kwaajili ya ujenzi huo.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa utoaji huduma kwa wananchi Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Bw.Stafa Nashoni ameipongeza Serikali ya Awamu ya tano kwa kufanikisha ujenzi wa hospitali hiyo kwaajili ya kusaidia wananchi wasiende kufuata huduma mbali.
Nashon ameeleza Zaidi kuwa jumla ya shilingi,bilioni 1.5 zimetumika kwaajili ya kukamilisha miundombinu na serikali imeongeza jumla ya shilingi milioni 300 kuendeleza ukamilishaji wa miundpombinu katka hospital.
“Tunamshukuru Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kutuletea fedha za ujenzi wa hospital ya wilaya na leo watu wanapata huduma.”
Aidha Bw.Nashonin amewashukuru wananchi wa kijiji cha Bukama kwakujitolea ardhi yao bure kwaajili ya ujenzi wa hospitali ,lakini pia ushiriako wanaoutoa wakati wa utekelezaji mradi huo.”asanteni na mbarikiwe”
Akiongewa kwa niaba ya wananchi wa Nyamswa Bw.John Nyamonge amesema tumeipokea hospital hii kwa mikono miwili na tupo tayari kushirikiana na watumishi kama ilivokua wakati wa ujenzi.
“Sisi kama wanajamii tunakazi moja ya kulinda hospital hii kw azote”
Tunatoa shukrani za Dhati kwa Serikali ya Awamu ya tano chini ya Dkt.John Pombe Magufuli kwa kutuletea huduma hii karibu.
Halmashauri ya Wilaya ya Bunda ina Hospital Moja , vya Afya vitano,na Zahati Ishirini na Sita.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda