• Malalamiko |
    • Maswali |
    • Barua Pepe |
Bunda District Council
Bunda District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Kilimo, Umwagiliaji & Ushirika
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji
      • Fedha & Biashara
      • Ujenzi
      • Afya
      • Mifugo & Uvuvi
      • Elimu Sekondari
      • Rasilimali Watu
      • Maendeleo ya Jamii
      • Usafi & Mazingira
      • Elimu Msingi
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ufugaji Nyuki
      • Uchaguzi
      • Manunuzi
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Elimu Msingi
    • Barabara
    • Mifugo
    • Afya
    • Mazao ya kilimo
  • Fursa za Uwekezaji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha, Uongozi & Mipango
      • Elimu, Afya & Maji
      • AIDS Control
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Uma
    • Video
    • Hifadhi ya Picha
    • Habari
    • Matukio

VIONGOZI SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA WILAYA YA BUNDA WAPEWA MAFUNZO YA UONGOZI ILI KUWAJENGEA UWEZO WA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO.

Posted on: January 3rd, 2025

Halmashauri ya Wilaya ya Bunda kwa kushirikiana na Ofisi ya   rais TAMISEMI na Chuo cha Serikali za Mitaa  Hombolo, wametoa mafunzo kwa viongozi wapya wa Serikali za Mitaa waliochaguliwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa wa tarehe 27 Novemba 2024. Mafunzo hayo yamefanyika siku ya tarehe 3/1/2025 katika shule ya Sekondari Mwibara.

Katika mafunzo hayo wamepata nafasi ya kupitia sheria mbalimbali zinazogusa majukumu yao ikiwemo sheria ya Serikali za mitaa sura ya 288 na 287,  sheria ya fedha na sheria nyingine, pia wamehimizwa kuimarisha umoja katika utendaji kazi wao.

Akifungua mafunzo hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Bw.George S. Mbilinyi amewataka viongozi hao kuwa na maadili ya kusimamia haki za wananchi na kusimamia shughuli zote za maendeleo zinazoendeshwa katika maeneo yao.Huku akiwakumbusha kushiriki katika ukusanyaji wa mapato kwa kutoa Elimu kwa wananchi katika maeneo yao.

"Zingatieni maadili ya kazi ilikuwa viongozi bora katika maeneo yenu lakini pia hakikisheni mnasimamia vizuri mapato yote ya Kijiji na Halmashauri ili kuleta maendeleo bora katika Halmashauri yetu". Amesema Bw.Mbilinyi.

Akitoa mafunzo hayo, Mhadhiri kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa maarufu kama Hombolo Ndugu Victor Mwinyipembe  kupitia somo la Uongozi na Utawala bora amesema kuwa nafasi zao za uongozi  ni kwa muujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wanapaswa kufuata muongozo wa katiba katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.

“Uongozi ni dhamana, mnapaswa kuwa watiifu na wanyenyekevu badala ya kuwa wenye mamlaka na madaraka na hili kuwa kiongozi bora nilazima kufuata sheria kama zinavyoelekezwa na katiba ya nchi, nilazima kuzingatia utawala bora kwa kuzingatia namna sahihi ya  utumiaji wa rasilimali ili kufikia malengo". Amesema Mwinyipembe.

Kwa upande wake Mhadhiri wa chuo cha Serikali za Mitaa Ismail Juma amewataka viongozi hao kuelewa majukumu yao ili kuepuka kufanya majukumu ya watu wengine na kuwahamasisha zaidi kufanya vikao vya mara kwa mara katika vijiji vyao pamoja na  kuwashirikisha wananchi na wataalamu katika maamuzi yeyote ya kimaendeleo ili kuepuka kuleta migogoro.

Hatahivyo mada zilizofundishwa zilihusu sheria, uongozi bora, usimamizi wa fedha, mipango ya maendeleo na udhibiti wa ardhi. Pia viongozi hao walitoa ahadi ya kusimamia haki na kuhakikisha miradi ya maendeleo inakamilika kwa wakati.

Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI KWA NAFASI ZA UDEREVA May 07, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO September 26, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI September 18, 2024
  • TANGAZO KWA WATUMISHI WOTE December 20, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU VYATEMBELEWA NA KUKAGULIWA NA KAMATI YA MIKOPO NGAZI YA HALMASHAURI

    April 26, 2025
  • WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA BUNDA WAHITIMISHA MAFUNZO YA SIKU 5 YA UANDAAJI NA UTENGENEZAJI WA MPANGO MKAKATI

    April 25, 2025
  • PROJECT ZAWADI YAIPIGA TAFU MASHINDANO YA UMITASHUMTA KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA BUNDA

    April 07, 2025
  • WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA BUNDA WAPEWA TUZO NA ZAWADI .

    April 03, 2025
  • Angalia zote

Video

Mvamizi wa eneo la soko.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Baraza la Madiwani
  • Dira na Dhamira
  • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Mpango Mkakati
  • Mpango wa Uwekezaji Sekta ya Samaki
  • Muundo wa Taasisi
  • OPRAS - Form

Viunganishi Muambata

  • Matokeo ya Darasa la Saba 2023 Bundadc
  • Matokeo ya darasa la saba
  • Matokeo ya darasa la saba
  • PO-RALG
  • PO-PSM
  • Matokeo ya Kidato cha Nne 2019

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Kibara Stoo.

    Anuani ya Posta: 126, Bunda

    Simu: 0282621055

    Hamishika: 0742163056

    Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda