• Malalamiko |
    • Maswali |
    • Barua Pepe |
Bunda District Council
Bunda District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Kilimo, Umwagiliaji & Ushirika
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji
      • Fedha & Biashara
      • Ujenzi
      • Afya
      • Mifugo & Uvuvi
      • Elimu Sekondari
      • Rasilimali Watu
      • Maendeleo ya Jamii
      • Usafi & Mazingira
      • Elimu Msingi
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ufugaji Nyuki
      • Uchaguzi
      • Manunuzi
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Elimu Msingi
    • Barabara
    • Mifugo
    • Afya
    • Mazao ya kilimo
  • Fursa za Uwekezaji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha, Uongozi & Mipango
      • Elimu, Afya & Maji
      • AIDS Control
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Uma
    • Video
    • Hifadhi ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Vikundi vya Watu wenye Ulemavu,Wanawake na Vijana Vyapatiwa Mafunzo

Posted on: April 11th, 2020

*VIKUNDI  VYA WATU WENYE ULEMAVU, WANAWAKE  NA VIJANA VYAPATIWA MAFUNZO.*

Halmashauri ya Wilaya ya Bunda kupitia Idara ya  Maendeleo ya Jamii imeendesha  mafunzo  ya mikopo isiyo na riba kwa vikundi vitakavyonufaika na  mkopo huo ikiwa  sambamba na Elimu ya ujazaji wa fomu za mikataba. Mafunzo hayo yametolewa Aprili 9, 2020 katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya Bunda.

Akizungumza wakati wa  mafunzo hayo  Kaimu Afisa Maendeleo ya Jamii  Bi.Beatrice Gwamagobe amesema mjasiriamali lazima awe Mbunifu ili kukuza na kuongeza thamani biashara anayoifanya.

”Tunategemea kama mkulima wa mpunga utakoboa utapata mchele na utauza pumba.” 

Amevitaka vikundi vyote vitakavyonufaika na  mkopo vihakikishe vinatumia fedha hizo kuendeleza  ujasiriamali ili kuepuka usumbufu wakati wa marejesho huku akisisitiza kuwa wabunifu wa mbinu mbalimbali zitakazo wawezesha kutoka hatua moja kimaendeleo kwenda nyingine.

“Ni wakati wa vikundi kufanya kazi kwa ushirikiano na kuongeza ubunifu ili  kuleta matokeo chanya katika kujikwamua kiuchumi na kutengeneza ajira kwa wengine.”

Kwa upande wake,  Afisa Maendele ya Jamii Msaidizi Bi. Liliani Mugwe ametoa rai kwa wanavikundi kufuata taratibu za kifedha kwa kufanya marejesho kwa wakati. 

"kila mwanakikundi anawajibu wa kufuata taratibu za  kurejesha mkopo. Hiyo itasaidia kujenga uaminifu na kusaidia kufikisha malengo ya kikundi. Mkumbuke baada ya kupata slip ya benki mnaleta ofisini hapa kwa ajili ya kupata uthibitisho kuwa marejesho yamepokelewa.” Amesema Liliani

Naye, Afisa vijana, Colmani Mushi amewataka wanavikundi hao  kutumia  fedha hizo kulingana na lengo.

 " Baada ya miezi mitatu tunategemea kila kikundi kitafanya marejesho ya mkopo. Ninyi viongozi mkasimamie hizi pesa. Tunategemea wote mtafanya vizuri ili kukuza kipato. kwa wakulima wa bustani kama mtapata nafasi mkatembelee Bulamba farmers wanajishughulisha na kilimo cha bustani na wanafanya vizuri sana”. Amesema Mushi.

Nao wanufaika wa mikopo hiyo wameishukuru serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na na Dkr. John Pombe Magufuli kwa kuendelea kuwajali na kuwawezesha wajasiriamali wadogo wadogo kwa kuwapatia  mkopo usio na riba  na wameahidi kutumia mkopo huo kwa lengo la kukuza shughuli zao za ujasiriamali na kutimiza lengo la serikali la kuwakwamua Wajasiriamali  kiuchumi.

Kwa Mwaka wa fedha 2019/2020 Halmashauri  ya  Wilaya ya Bunda imetoa kiasi Cha shilingi milioni20 kwa vikundi  vya wanawake,watu wenye ulemavu na Vijana  kwa awamu hii ya pili Halmashauri inatarajia kutoa jumla ya shilingi milioni 30 kwa vikundi 13 ikiwa  vikundi 3 vya  walemavu, vitano vya  vijana na 5 kwa wanawake. Mikopo  hiyo inatolewa kwa mujibu wa sheria na miongozo inayoelekeza Mapato ya ndani ya Halmashauri kutolewa mkopo isiyokua na riba kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI KWA NAFASI ZA UDEREVA May 07, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO September 26, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI September 18, 2024
  • TANGAZO KWA WATUMISHI WOTE December 20, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU VYATEMBELEWA NA KUKAGULIWA NA KAMATI YA MIKOPO NGAZI YA HALMASHAURI

    April 26, 2025
  • WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA BUNDA WAHITIMISHA MAFUNZO YA SIKU 5 YA UANDAAJI NA UTENGENEZAJI WA MPANGO MKAKATI

    April 25, 2025
  • PROJECT ZAWADI YAIPIGA TAFU MASHINDANO YA UMITASHUMTA KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA BUNDA

    April 07, 2025
  • WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA BUNDA WAPEWA TUZO NA ZAWADI .

    April 03, 2025
  • Angalia zote

Video

Mvamizi wa eneo la soko.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Baraza la Madiwani
  • Dira na Dhamira
  • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Mpango Mkakati
  • Mpango wa Uwekezaji Sekta ya Samaki
  • Muundo wa Taasisi
  • OPRAS - Form

Viunganishi Muambata

  • Matokeo ya Darasa la Saba 2023 Bundadc
  • Matokeo ya darasa la saba
  • Matokeo ya darasa la saba
  • PO-RALG
  • PO-PSM
  • Matokeo ya Kidato cha Nne 2019

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Kibara Stoo.

    Anuani ya Posta: 126, Bunda

    Simu: 0282621055

    Hamishika: 0742163056

    Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda