• Malalamiko |
    • Maswali |
    • Barua Pepe |
Bunda District Council
Bunda District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Kilimo, Umwagiliaji & Ushirika
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji
      • Fedha & Biashara
      • Ujenzi
      • Afya
      • Mifugo & Uvuvi
      • Elimu Sekondari
      • Rasilimali Watu
      • Maendeleo ya Jamii
      • Usafi & Mazingira
      • Elimu Msingi
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ufugaji Nyuki
      • Uchaguzi
      • Manunuzi
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Elimu Msingi
    • Barabara
    • Mifugo
    • Afya
    • Mazao ya kilimo
  • Fursa za Uwekezaji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha, Uongozi & Mipango
      • Elimu, Afya & Maji
      • AIDS Control
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Uma
    • Video
    • Hifadhi ya Picha
    • Habari
    • Matukio

UFAULU KWA KIDATO CHA NNE KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA BUNDA WAONGEZEKA KWA ZAIDI YA ASILIMIA 90.

Posted on: February 12th, 2025

Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mh.Dkt Vicent Anney ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Bunda kwa kupanda kwa kiwango cha ufaulu Katika matokeo ya mitihani ya kidato cha nne kwa mwaka wa masomo 2024/2025 kutoka asilimia 85 hadi 94% ikilinganishwa na mwaka uliyopita, huku akiwahimiza kuongeza juhudi zaidi  katika upande wa elimu ili kuondoa matokeo mabovu katika halmashauri hiyo.

Pongezi hizo amezitoa siku ya tarehe 12/02/2025 katika kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda uliopo Kibara stoo.

Amesema matokeo ya kidato cha nne kwa mwaka huu yanatia matumaini na yanaonyesha namna gani Halmashauri  imeanza kupiga hatua katika upande wa elimu.

"Matokeo ya mwaka huu yanaonyesha njia ni kwa namna  gani tumeanza kupiga hatua ukilinganisha  na mwaka uliopita hivyo niwasihi kuendelea na kasi hii ili kuendelea kuimarisha zaidi sekta yetu ya elimu  katika Halmashauri na Wilaya nzima ya Bunda.  "Amesema Dkt Anney

Aidha, Mh.Dk Anney amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda kuongeza kasi na juhudi za ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri ili kufikia malengo kama mwaka wa fedha uliopita na  kuwasisitiza watumishi  wa umma kusimamia majukumu yao kwa kuzingatia kanuni, sheria na utaratibu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Bw. George S. Mbilinyi amesema, ongezeko la ufaulu kwa matokeo ya kidato cha nne limechochewa na uhamasishaji, uboreshwaji wa miundombinu ya elimu pamoja juhudi kubwa na ushirikiano kati ya wataalamu wa elimu kutoka Halmashauri, walimu pamoja na wananchi kwa namna walivyojitoa katika kuchangia mambo mbalimbali ikiwemo chakula kwa wanafunzi shuleni.

Ameongeza kuwa licha ya kuongezeka kwa ufaulu wa matokeo ya kidato cha nne lakini bado kumekuwa na changamoto katika baadhi ya maeneo na wao kama Halmashauri wamekuwa wakiendelea kutafuta utatuzi wa changamoto hizo pamoja na kutoa hamasa ili kuendelea kufanya vizuri zaidi Katika sekta ya elimu katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAHILI June 04, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO September 26, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI September 18, 2024
  • TANGAZO KWA WATUMISHI WOTE December 20, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • ELIMU YA UTUNZAJI NA UHIFADHI WA MAZINGIRA YATOLEWA KWA WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI MWIBARA

    June 04, 2025
  • ZIARA YA MKUU WA WILAYA YA KUTEMBELEA NA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO

    June 03, 2025
  • ELIMU IENDELEE KUTOLEWA KWA VIJANA RIKA BALEHE.

    May 31, 2025
  • WAUGUZI KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA BUNDA WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI

    May 30, 2025
  • Angalia zote

Video

Mvamizi wa eneo la soko.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Baraza la Madiwani
  • Dira na Dhamira
  • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Mpango Mkakati
  • Mpango wa Uwekezaji Sekta ya Samaki
  • Muundo wa Taasisi
  • OPRAS - Form

Viunganishi Muambata

  • Matokeo ya Darasa la Saba 2023 Bundadc
  • Matokeo ya darasa la saba
  • Matokeo ya darasa la saba
  • PO-RALG
  • PO-PSM
  • Matokeo ya Kidato cha Nne 2019

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Kibara Stoo.

    Anuani ya Posta: 126, Bunda

    Simu: 0282621055

    Hamishika:

    Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda