Kama moja ya hatua ya utekelezaji wa mradi wa Uboreshaji wa Mifumo katika Sekta ya Umma (PS3), shughuli ya kusimika miundombinu ya mtandao kiambo (LAN) imekamilika katika halmashauri ya Wilaya ya Bunda. Shughuli hii iliyoendeshwa na timu ya wataalamu toka Ofisi ya Rais TAMISEMI na PS3 kupitia ukandarasi wa kampuni ya SoftNet imefanyika katika ofisi za Mkurugenzi Mtendaji (W), Mipango, TEHAMA, Rasilimali Watu, Fedha na Manunuzi ambao kwa sasa ndio wadau wakuu katika matumizi ya mifumo iliyopo ya TEHAMA kama vile IFMIS, HCMIS, LGRCIS, PlanRep, TASAF-MIS na GSPP.
Uboreshaji huu wa miundombinu ya Mifumo ya TEHAMA utasaidia sana katika kuongeza ufanisi wa mifumo hiyo kwani ilikuwa inakabiliwa na changamoto kubwa ya uchakavu wa miundombinu inayoihudumia na hivyo kupunguza ufanisi wake. Ili kuhakikisha kuwa zoezi hili linafanikiwa kama ilivyopangwa, Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji imeshiriki kutatua changamoto zilizojitokeza kama vile upungufu wa vitendea kazi, vifaa na nguvu-kazi.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji (W) inatoa shukrani za pekee kwa uwezesho huu toka PS3 (kwa niaba ya Watu wa Marekani), Kampuni ya SoftNet na usimamizi wa Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Makao Makuu katika kuhakikisha kuwa malengo ya mradi husika yanafikiwa.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda