Kamishina wa Elimu Wizara ya Elimu amezindua Maktaba Nane za mfano zenye gharama ya shilingi milioni 240,959,579 zilizojengwa na Shirika lisilo la Kiserikali Project Concern Internation (PCI) Kwakushirikiana na Halmashuri, serikali ya kijiji Halmashauri ,pamoja na Wananchi wa Mkoa wa Mara.
Akizingumza kwa niaba ya Kamishina Bwa. Victor Bwindiki Mdhibiti Mkuu Ubora Kanda ya Ziwa katika ghafla ya uzinduzi wa Maktaba iliyopo Shule ya Msingi Nyamitwebili Disemba 17, 2020.
Bwa.Bwindiki ametoa pongezi kwa PCI kwa kazi nzuri waliofanya kujenga Maktaba itakayoleta manufaa kwa kizazi cha sasa na baadae.
Bwa. Bwindiki ametoa wito kwa walimu kuhakikisha uwepo wa utaratibu mzuri wa kuingia Maktaba kwaajili ya kujisomea ili waendelee kutunza vitabu pamoja na thamani zilizopo.
“Niwajibu wa Walimu kusimamia utunzaji wa Maktaba naamini kupitia maktbaa hii itasaidia hata wadau wanaofanya tafiti kuweza kupata taarifa mbalimbali ili kukamilisha tafiti zao.”Alisema Bwindiki
Aidha Bw.Bwindiki amewataka wazazi kuhakikisha watoto waliofikisha umri wa kwenda shule wanaenda.
“kama mzazi niwajibu nia wajibu wako kuhakikisha mtoto aliyefikisha umri wa kwenda shule unamuandikisha ilikuendelea kukuza vizazi vyenye elimu”alisema Bwindiki
Bwa. Bwindiki aliendelea kuipongeza Shirika la PCI kwa kutoa chakula Shuleni kwa kipindi cha Miaka Kumi ambapo mpaka sasa imesaidia kuleta hamasa kwa wazazi kuchangia chakula shuleni.
“PCI imeonesha umuhimu wa chakula shuleni hata walipositisha kutoa huduma ya chakula wazazi wanaendelea.”alisema Bwindiki
Naye ,Susana Nyarubamba Mkurugenzi msaidizi wa Elimu TAMISEMI amesema Serikali imejipanga kikamilifu katika kuweka mazingira bora ya kujifunza na kufundishwa,huku akisisitiza kila mwananchi kuwa mlinzi wa mwenzake katika kulinda miradi inayotekelezwa na iliyokamilika.
“Maktaba hii itakuja kutumika na vizazi na vizazi hivyo PCI wameacha alama.”Alisema Bi.Nyarubamba
Katibu Tawala mkoa Bi. KarolinaMthapula amewahasa wananchi kuendelea kuhamasisha wazazi watumie muda mwingi kuangalia maendeleo ya Elimu kwa Watoto.
Pamoja na hayo Bi.Mthapula ametoa rai kwa walimu kusimamiz vizuri maendeleo ya wanafunzi darasani ilikujenga kizazi chenye tija.
“Walimu hakikisheni kuiwa wanafunzi wanasoma kwelikweli na vitabu vya maktaba sio mapambo”alisema Mthapula
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Miradi PCI Bi Amina Mgeni ametoa shukrani kwa Ngazi ya kijiji,Halmashauri,mpaka mkoa kwakuendelea kutoa sapoti kama wadau.
Aidha Bi Mgeni ametoa wito kwa jamii na viongozi kuwa kinachofanya na Shirika ni kwaajili yetu sisi wananchi na sio wazungu wazazi na walezi tuendelee kushikama kwa pamoja katika kuhimiza watoto kusoma pamoja na kutumia maktaba kwa manufaa ya sasa na baadae.
“Binafsi nimejifunza kusoma katika maktaba na sio darasa hivyo wazazi tuwe mstari wa mbele kuhamasisha watoto kusoma”alisema Bi mgeni
Bi Mgeni alieleza zaidi kuwa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Dkt John Pombe Magufuli inaendelea kuwathami wananchi wake kwakuweka mazingira bora ya kujifunza sisi kama wadau wa Elimu hatuna budi kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais.
“Tumuunge mkono mhe Rais kwa kufanya uyote yale anayoyasema na sisi kama viongozi tuwe walinzi na kusimamia vya kwetu”.alisema Bi Mgeni
Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mhe Lydia Bupilipil pia ametoa pongezi kwa Shirika la PCI kwakuwatendea wananchi haki na kuenedelea kushirikiana na Serikali katika kuchangia katika miradi ya maendeleo ya elimu hasa katika kuboresha miundombinu .
“Kulikua na wanafunzi ambao hawapendi kwenda shule lakini siku hadi siku kutokana na jitihada za serikali na wadau wanafunzi hao wanahamasika kusoma”.alisema Bupilipili
Naye,Mwekiti wa Kijiji cha Nyamwitebili Bwa.Masambu ametoa shukrani kwa Shirika la PCI kwa kuendelea kuuonga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano nakuahidi kuendelea kutunza na kuthamini miundombinu yote iliwekwa katika maktaba na mazingira ya shule kwa ujumla.
Kwa hatua nyingine Bwa.Bwindiki alikagua mradi wa maji ya kisima unaosukumwa kwakutumia sola uliojengwa na PCI katika shule ya Msingi Busambara ambapo Mradi huo uligharimu kiasi cha shilingi milioni 43.6.
Mbali na utoaji wa Chakula shuleni kwa kipidi cha Miaka Kumi,PCI pia imejikita katika kutoa mafunzo kwa walimu,vitabu kwa wanafunzi pamoja na kutoa mafunzo kwa jamii ili kujenga uhusiano mzuri kati ya mwalimu,mzazi na mwanafunzi
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda