Mwenge wa Uhuru wa Mwaka 2017 umezindua miradi ipatayo mitatu (3) katika halmashauri ya Wilaya ya Bunda baada ya Mwenge huo kutua Mkoani Mara ukitokea Mkoani Mwanza, Wilayani Ukerewe na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Mara Dr. Charles Mlingwa. Halmashauri ya Wilaya ya Bunda imekuwa halmashauri ya kwanza katika Mkoa wa Mara kupokea Mwenge huo tayari kuanza mbio zake mkoani hapa.
Mara baada ya Mkuu wa Mkoa wa Mara kuupokea Mwenge huo toka kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Ndg. John Mongella, aliukabidhi kwa Mkuu wa wilaya ya Bunda Ndg. Lydia Bupilipili ambaye naye aliukabidhi kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Ndg. Amos Kusaja ambapo Mwenge huo ulikimbizwa maeneo mbalimbali ya halmashauri hii na kuweza kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi mbalimbali ikiwemo Jengo la Mganga wa Zahanati ya Nansimo, Mradi wa Maji wa Kibara na jengo la Hosteli ya Wasichana, shule ya Sekondari Makongoro.
Kauli mbiu iliyobebwa na Mwenge huo wa Mwaka 2017 ni "SHIRIKI KUKUZA UCHUMI WA VIWANDA KWA MAENDELEO YA NCHI YETU" ambapo miongoni mwa mambo yanayosisitizwa ni pamoja na Kupambana na Madawa ya Kulevya, Ushiriki wa Wananchi katika kukuza Uchumi kupitia Viwanda, Mapambano dhidi ya UKIMWI na Kutokomeza Mimba za Utotoni.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda