Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Bi.Changwa Mkwazu amewataka Watendaji Kata,Maafisa Elimu Kata ,Walimu Wakuu na Waganga wafawidhi kufanya kazi kwa uwajibikaji Ili kukamilisha miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao.
Hayo amesema Oktoba 20, 2021 katika kikao cha kuweka mikakati ya kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya Uviko-19 kupitia fedha zilizoletwa na Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan.
Bi.Mkwazu amewataka Waganga Wafawidhi ,Walimu wakuu na Watendaji Kata kuepuka majaribu yeyote yatakayo kwamisha kufanikisha kwa utekelezaji wa miradi hiyo.
“Rushwa,Uzembe na kutojali miradi husababisha miradi kukwama,Ofisi ya Mkurugenzi haitamvumila yeyote atakayekwamisha miradi isiendelee’'amesema Bi.Mkwazu
Aidha Bi.Mkwazu amesisitiza kuwa miradi inatikiwa kuisha kwa haraka na kuwa na viwango kwa kuzingatia miongozo ya Force Akaunti.
“Nasisitiza kufuata taratibu zote za manunuzi pamoja na utunzaji wa nyaraka hii itasaidia hata katika ukaguzi"amesema Bi.Mkwazu
Naye , Bertha Sayi Mwalimu Shule ya Sekondari Salama ametoa shukrani ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda kwa kutoa uelewa wa pamoja wa namna yakufanikisha kutekeleza miradi ya maendeleo.
“kupitia kikao hiki naamini wote tutafanikiwa kwa pamoja"amesema Mwal.Sayi
Mwalimu Bertha ametoa rai kwa Walimu Wakuu wengine,Watendaji Kata na Waganga wafawidhi kushirikiana na kuwajibika ili kuhakikisha miradi inakamalika kwa viwango vya hali ya juu
“Ni wajibu wetu kufanya kazi kama timu ili tuweze kufanikiwa,sambamba na hilo tuweke wazi hali ya mapato na matumizi ili kuepusha migogoro na Wananchi “amesema Mwal.Bertha
Kwa hatua ingine Bi.Mkwazu ametoa Shukrani kwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe.Samia Suluhu Hassan kwakutoa Tshs. 2,550,000,000 fedha kwaajili ya ujenzi wa miundombinu ya vyumba vya madarasa 67, ujenzi wa jengo la huduma za dharura,ujenzi wa jengo la ICU na Nyumba za Watumishi naTshs.250,000,000 zilizotokana na Tozo ya mialama ya simu kwaajili ya ujenzi wa kituo cha afya Kijiji cha Isanju kata ya Iramba.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda