Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mhe. Lydia Bupilipili amesema moja ya vipaumbele vya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuhakikisha kwamba wananchi hasa wa sekta zisizo rasmi wanapata matibabu kupitia Mfuko wa Bima ya Afya ya Jamii iliyoboreshwa.
Mhe. Bupilipili ameyasema hayo leo wakati wa Uzinduzi wa Mfuko wa afya ya jamii iliyoboreshwa katika kata ya Nyamuswa Kijiji cha Nyamuswa,alieleza zaidi kuwa Serikali ya awamu ya Tano imehakikisha kuwa huduma ya afya inawafikia wananchi wote haswa wenye kipato cha chini.
“Serikali ina nia ya kumfikia kila Mtanzania na kumpatia huduma bora za afya”.
Aidha Mhe Bupilipili amewataka wananchi wa Halamshauri ya Wilaya ya Bunda kuweka kiapaumbele na kuzingatia afya zao kwakujiunga na Mfuko wa afya ya jamii iliyoboreshwa ili kuweza kuwasaidia pindi wanapopatwa na changamoto ya ugonjwa.
“ Natoa maelekezo na kuagiza kuwa kila kiongozi wa kijiji kuhakikisha kaya zilizomo katika kijiji chake zinajiunga na mfuko wa ya afya ya jamii iliyoboreshwa ili kuwa na uhakika wa matibabu hata wakati hana fedha.”
“Mganga Mkuu wa Halmashauri na Mratibu wa afya ya jamii iliyoboreshwa hakikisheni mnfanya hamasa ya kwa wananchi ili waweze kujiunga na mfuko wa ya jamii iliyoboreshwa”.
‘’Ugonjwa hauna tabia ya kutoa taarifa kuwa tarehe fulani utamkumba mtu fulani.unakuja bila matarajio ya mhusika.hii ni ni hatari kwa usalama wa mtu huyo endapo ugonjwa utamkuta hajajiunga na mfuko wa afya ya jamii iliyoboreshwa.”amesema Mhe Bupilipili
Kwa upande wake Kaimu mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Bunda Bw.Stafa Nashon ameishukuru serikali ya Awamu ya Tano Chini ya Dkt John Pombe Magufuli kwa kufanya mambo makubwa katika upande wa afya kwakuweka miundombinu bora na pamoja kuanzisha kwa mfuko wa afya ya jamii iliyoboresha.
“serikali hii imewajali wananchi na imetimiza wajibu wake wakuhakikisha jamii inapata huduma ya afya iliyobora”.alisema
Naye, Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Bw.Nuru Yunge amesema kuwa huduma ya afya ya jamii gharama zimeongezeka kutoka elfu kumi hadi elfu thelathini lakini pia huduma zimeongezeka awali mwanachama alikuwa anatibiwa katika kituo cha afya alichojiandikishia lakini sasa hivi ukishalipia hiyo elfu Thelathini(30) utatibiwa popote ndani ya Mkoa wa Mara,hivyoUkitoa elfu Thelathini utatibiwa familia nzima ya watu sita kwa mwaka mzima katika hospitali yeyote ndani ya Mkoa.
“Lengo la Serikali ni Kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya.”
Wakati huo huop,Bi. Bhoke Makongoro Mkazi wa Kijiji cha Nyamuswa amesema mfuko huo wa afya ya jamii iliyoboreshwa umesaidia mno kupunguza gharama kubwa za matibabu kwa sasa.
“sasa hivi sisi wananchi wenye kipato cha chini, si rahisi kumudu gharama za ,matibabu zinazotozwa na vituo vya kutolea hudumu za afya.lakini ukiwa na bima ya afya jamii,hata kama fedha huna unauhakika wa kupata matibabu ya gharama yoyote”amesema Makongoro
Mfuko wa afya ya jamii ilianzishwa rasmi Mwaka 2001 ilivoanzishwa kwa sheria Mfuko wa afya ya Jamii kwa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda tangu Februari mwaka huu iimeanza kutumia mfuko wa afya ya jamii na kaya 301 zimejiandikisha na huku kaya 43458 zinategemea kujiandikisha katika mfuko huo.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda