Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mhe.Joshua Nassari amewataka Wananchi wa Bunda kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Virusi vya Korona (UVIKO-19).
Mhe Nassari ametoa kauli hiyo Julai 22,2021 katika kikao cha Kamati ya Afya ya Msingi ya Wilaya kilichofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya uliopo Bunda Mjini.
‘’Hatuwezi kuzui ibada zisifanyanyike,nichukue fursa hii kuendelea kuwasisitiza viongozi wa dini kuhakikisha waumini wanachukua tahadhari kwa kuhakikisha uwepo wa maji ya kunawa mikono,kuvaa barakoa pamoja na kuachiana nafasi ’’amesema Mhe.Nassari
Katika Kikao hicho Mhe Nassari alipokea Taarifa ya Tathimini ya sita ya utekelezaji wa afua za Lishe kwa Mwaka 2020-2021.
Akitoa wasilisho hilo Afisa Lishe wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Bwa. January Dalushi amesema kuwa asilimia 32 ya watoto chini ya miaka 5 Tanzania wamedumaa na hawana uwezo wa kufundishika. Kwa Wilaya ya Bunda asilimia 29 ya Watoto chini ya miaka 5 wamedumaa, asilimia 5.3 wana utapiamlo wa kadri, asilimia 0.5 ya watoto wanaozaliwa wana uzito pungufu, asilimia 4.1 wana ukondefu, aidha asilimia 3.7 ya akina mama wenye umri wa kuzaa wanaupungufu mkubwa wa damu.
Bwa Dalushi alitaja mpango mkakati wa mwaka 2021-2022 ikiwa ni pamoja na kupanga bajeti kwaajili ya utekelezaji wa afua za lishe kiasi cha TSH,72,154,350 sawa na Tsh.1,117 kwa kila mtoto chini ya miaka 5 kwa Bunda DC na Tsh. 27,179,351 sawa na Tsh 888.7 kwa Bunda TC, Kutoa mafunzo ya lishe, kuongeza upatikanaji wa dawa na vifaa tiba, kuhamasisha jamii kupitia klabu za afya na lishe mashuleni na kufanya tathimi za lishe kila robo mwaka katika ngazi zote.
Kwa upande wake Mhe.Nassari ametoa agizo kwa Maafisa Elimu Sekondari na Msingi kuhakikisha kuwa shule zote zinaasha klabu za lishe.
‘Shule zote zianzishe klabu za lishe ili kutoa hamasa kwa jamii na kutambua umuhimu wa lishe bora’’amesema Mhe Nassari.
Pia Mhe Nassari alipokea Taarifa ya utekelezaji wa utoaji wa tiba kinga ya magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele
Akiwasilisha taarifa hiyo Dkt. Allan James alitaja walengwa wa zoezi hilo walikuwa ni wanafunzi wote wakike na wakiume wenye umri wa miaka 5 hadi 14.
Dkt James amebainisha idadi ya waliomeza kinga tiba ni 61383 sawa na asilimia 84 kwa halmashauri ya Wilaya ya Bunda na 49,500 sawa na aslimia 94 kwa Halmashauri ya Mji.
Mwisho Nassari alitoa rai kwa wajumbe wa kamati ya Afya ya Msingi kuendelea kuhamasisha wananchi kujenga vyoo pamoja na kutunza mazingira ili kuepuka magonjwa ya mlipuko.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda