• Malalamiko |
    • Maswali |
    • Barua Pepe |
Bunda District Council
Bunda District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Kilimo, Umwagiliaji & Ushirika
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji
      • Fedha & Biashara
      • Ujenzi
      • Afya
      • Mifugo & Uvuvi
      • Elimu Sekondari
      • Rasilimali Watu
      • Maendeleo ya Jamii
      • Usafi & Mazingira
      • Elimu Msingi
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ufugaji Nyuki
      • Uchaguzi
      • Manunuzi
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Elimu Msingi
    • Barabara
    • Mifugo
    • Afya
    • Mazao ya kilimo
  • Fursa za Uwekezaji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha, Uongozi & Mipango
      • Elimu, Afya & Maji
      • AIDS Control
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Uma
    • Video
    • Hifadhi ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mhe Lydia Bupilipili azindua Utoaji wa Chanjo ya Mifugo Dhidi ya Magonjwa ya Kipaumbele

Posted on: May 19th, 2021

Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mhe Lydia Bupilipili  amewataka wafugaji wa Mifugo katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda kuchangamkia fursa ya chanjo ya mifugo  iliyotolewa na Serikali kwa bei elekezi  ya shilingi mia tano na hamsini(550).

Hayo yamesemwa wakati wa uzinduzi wa  chanjo ya homa ya mapafu Mei 19,2021 katika Kijiji cha Sarakwa Kata ya Hunyari, Tarafa ya Chamriho.

Mhe Bupilipili alisema kuwa  lengo la Serikali kuinua kipato cha  wafugaji  kutokana na kuuza mifugo na mazao yake iliyo bora ndani na nje ya nchi pamoja na kuinua uchumi wa nchi.

“Sekta ya mifugo ni sekta ya tatu katika  kutupatia mapato katika nchi, hivyo ni vyema kwa wafugaji kuzingatia taratibu za ufugaji ili kuinua kipato cha mfugaji na nchi kwa ujumla’’alisema Bupilipili

Aidha Mhe Bupilipili ametoa rai kwa viongozi kuanzia ngazi ya kijiji na Halmashauri kuhakikisha wafugaji wote wanatekeleza agizo la kupeleka mifugo kupata chanjo na atakae kaidi hatua zaidi zichukuliwe.

“Kila kiongozi anawajibu wakuhakikisha kuwa zoezi hili linafanikiwa kwa asilimia mia na kwa mfugaji atakae kaidi hatua zaidi zichukuliwe’’.alisema Bupilipili

Kwa Upande wake Afisa mifugo,Bi Mary Luseke alisema kuwa  zoezi la utoaji wa chanjo kwa mifugo dhidi ya magonjwa kipaumbele  litafanywa na Wataalamu wa mifugo kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Bunda na kusimamiwa na Watalaamu kutoka wizara ya mifugo.

Bi.Luseke alibainisha magonjwa ya Kipaumbele kwa Mifugo ni Homa ya mapafu ya Ngo’mbe,Homa ya mapafu ya Mbuzi,Sotoka  ya mbuzi na kondoo,Ugonjwa wa miguu na midomo,Chambavu,Kimeta,Mapele ya Ngozi,Ndigana kali,Bonde la Ufa,Kichaa cha Mbwa,Kideri,Kutupa Mimba na Sotoka.

Bi Luseke alieleza Zaidi  kuwa  chanjo itakayoanza ni ya Homa ya mapafu ya Ng’ombe  

‘’Jumla ya Ng’ombe 131.250 wenye umri kuanzia  miezi sita na kuendelea watachanjwa kwa Mwaka 2020/2021’’.alisema Bi Luseke

Naye,Mwenyekiti wa Kijiji cha Sarakwa Bwa. Giragu Nyamurunga kwa niaba ya Wafugaji alishukuru Serikali kwakuwajali wafugaji katika kuwapelekea chanjo  ili kuimarisha Mifugo yao.

Halmashauri ya Wilaya ya Bunda ina jumla ya Ng”ombe  ya  173,502 ambao wanatengemewa kuchanjwa kulingana na magonjwa ya kipaumbele na zoezi hili la utoaji chanjo kwa Ng’ombe litadumu takribani siku Kumi na Tano.

Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI KWA NAFASI ZA UDEREVA May 07, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO September 26, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI September 18, 2024
  • TANGAZO KWA WATUMISHI WOTE December 20, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU VYATEMBELEWA NA KUKAGULIWA NA KAMATI YA MIKOPO NGAZI YA HALMASHAURI

    April 26, 2025
  • WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA BUNDA WAHITIMISHA MAFUNZO YA SIKU 5 YA UANDAAJI NA UTENGENEZAJI WA MPANGO MKAKATI

    April 25, 2025
  • PROJECT ZAWADI YAIPIGA TAFU MASHINDANO YA UMITASHUMTA KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA BUNDA

    April 07, 2025
  • WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA BUNDA WAPEWA TUZO NA ZAWADI .

    April 03, 2025
  • Angalia zote

Video

Mvamizi wa eneo la soko.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Baraza la Madiwani
  • Dira na Dhamira
  • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Mpango Mkakati
  • Mpango wa Uwekezaji Sekta ya Samaki
  • Muundo wa Taasisi
  • OPRAS - Form

Viunganishi Muambata

  • Matokeo ya Darasa la Saba 2023 Bundadc
  • Matokeo ya darasa la saba
  • Matokeo ya darasa la saba
  • PO-RALG
  • PO-PSM
  • Matokeo ya Kidato cha Nne 2019

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Kibara Stoo.

    Anuani ya Posta: 126, Bunda

    Simu: 0282621055

    Hamishika: 0742163056

    Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda