Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mhe Lydia Bupilipili ambaye pia ni Mwenyekiti wa Afya ya Msingi (PHC) alipokea taarifa ya Utekelezaji wa Zoezi la ugawaji wa kinga dawa kwa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele.
Akizungumza wakati wa upokeaji wa taarifa hiyo wa namna zoezi la ugawaji wa kinga dawa litakavyo tekelezwa Mei,2021 katika ukumbi wa Halmashauri ,Mhe Bupilipili alisema kabla ya zoezi kuanza ni muhimu kuweka uelewa wa pamoja kwa kutoa Elimu kwa jamii ili kuweza kupata ushirikiano zaidi na kuweza kupata mafanikio katika zoezi hili.
“kumekuwa na mitazamo hasi kwa jamii hasa inapotokea mazoezi kama haya ya uotaji chanjo,ni vyema elimu ikatolewa kwa Jamii.’’
Mhe Bupilipi alitoa msisitizo kwa mratibu wa zoezi kuhakikisha kuwa watoto watakaohusika kupata kinga dawa wapate chakula kabla ya kupata dawa ili watoto hao wasije zimia au kukosa nguvu baada ya kumeza dawa.
‘Dawa hizi imeonekana zinahitaji mtoto ashibe ndio apate dawa Walimu,na jamii kwa ujumula ione umuhimu wa uwepo wa chakula wakati wa zoezi hili’.alisema Mhe Bupilipili
Kwa Upande wake Mratibu wa Afya ya Msingi (PHC)Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Dkt Allan James alitaja magonjwa hayo kuwa ni Kichocho,Minyoo ya Tumbo,Trakoma,Matende,Mabusha pamoja na usubi yamekuwa yakiwapata watu, kwa awali magonjwa hayo yalikuwa hayakutiliwa mkazo kama magonjwa mengine.
“Serikali kupitia Wizara ya Afya imeona umihimu wa kutoa kinga dawa kwa Magonjwa haya sambamba na kutoa elimu juu ya utunzaji wa mazingira ili kuepusha jamii kuathirika’.
Dkt Allan alisema kuwa zoezi la kinga dawa linakusudiwa kugawa dawa za minyoo kwa watoto kuanzia umri wa miaka mitano mpaka kumi na minne katika shule za Msingi 104 zilizopo Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.
“Zoezi hili litahusisha watoto wote walikuwa shuleni na wasiokuwa shuleni ilimradi awe katika umri wa miaka mitano mpaka kumi na minne’’alisema Dkt Allan
Mwaka 2018 zoezi la utoaji kinga dawa lilifanikiwa kwa asilimia 90 na jumla ya kiasi cha shilingi 43,044,751 kilitumika na kwa Mwaka 2021 zoezi linategemea kutumia kiasi cha shilingi 25,144,000 na linategemea kufikia jumla ya watoto 7375.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda