Mkuu wa Wilaya yaBunda Mh Lydia Bupilipili amehamasisha wananchi wa Kata ya Nyamihyolo kujenga Shule ya Sekondari ambapo ujenzi huo utagharamiwa na nguvu za Wananchi wa Kata hiyo katika kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya tano chini ya Dkt.John Pombe Magufuli.
Akizungumza katika Mkutano wa hadhara Januari8,2020 katika eneo la Nyamitwebili alisema ilikujenga kizazi bora lazima kuwepo na msingi mzuri wa elimu kwa kizazi tulichonacho ambacho kitaleta manufaa ya sasa na baadae.
Wanafunzi wanatembea umbali mrefu kufuata Shule,hivyo nawaagiza wananchi wa Nyamihyolo kupeleka nguvu kazi katika ujenzi wa shule ya Sekondari ya kata ili wanafunzi wasitembee umbali mrefu.alisema Bupilipili
Pamoja na changamoto zilizokuwepo baina ya Wananchi wa Nyamihyolo kuhusu eneo ambalo litajengwa Shule ya Sekondari,pia Mh Bupilipili aliwasihi Wananchi hao kumaliza mgogoro wao kwa haraka ili kuweza kukamalisha ujenzi huo.
Naye ,Afisa Elimu Bwa.sylvester A.Mrimi aliwahimiza wazazi kuendelea kuhamasika kupeleka watoto wakike shule ili kuwajengea maisha bora ya baadae.
" Wananchi wa Nyamihyolo endeleni kutoa hamasa kwa ujenzi wa Shule ili uweze kukamilika kwa haraka."kama kuna familia ipo hapa haifikirii mtoto wake kupata maarifa basi mzazi huyo hapendi maendeleo ya mtoto wake"
Madarasa manne yatasaidia kuanzia ili watoto wakidato Cha kwanza waweze kusoma.alisema afisa elimu.
Aidha,Kaimu Katibu tawala wa Wilaya Bwa.Jonas Nyehoji alisema umoja Ni nguvu utengani ni udhaifu ni vyema kuunganisha nguvu kwa pamoja ili kuweza kuhakikisha ujenzi wa Shule unakamalika kwa haraka ili watoto waanze kutumia madarasa hayo.
Pia Mh Bupilipili alitoa agizo la kusitishwa kwa ujenzi wa Shule ya Sekondari Nyamitwebili kutokana na kutokidhi vigezo vya kua eneo la shule kwa kuwepo na mgogoro wa eneo hilo.
akaelekeza vifaa vyote vilivyotolewa kwa ajili ya ujenzi wa Shule hiyo vipelekwe eneo la Mihyolo ambalo Shule itajengwa, viongozi kutoa mrejesho wa vikao ambavyo wanawakilisha Wananchi ili kuondoka sitofahamu kwa Wananchi na watalaamu wa Halmashauri wakishirikiana na wakaguzi wa ubora wa shule kufanya tathmini upya ya maeneo yaliyopendekezwa kujengwa Shule.
Kata ya Nyamihyolo ina vijiji vitatu ambavyo ni Nyamitwebili,Mahyolo na Haluzale pamoja na vitongoji 12 vyenye watu takribani5000.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda