Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, Ndugu George S. Mbilinyi siku ya tarehe 4/5/2024 alifanya mkutano na wananchi wa kijiji cha Kurusanga, kilichopo Kata ya Salama katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.
Mkurugenzi Mtendaji alisema, lengo la mkutano huu ni kusilikiza kero na changamoto mbalimbali mnazokabiliana nazo na kuona namna ya kuzitatua, leo hii nimekuja na baadhi ya wakuu wa idara kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Bunda ambao nao watakuwa sehemu ya kutatua kero hizo.
Wanakijiji cha Kurusanga walimpongeza Mkurugenzi Mtendaji kwa hatua na maamuzi aliyoyafanya kwa kuja kuwatembelea na kukubali kuwasikiliza kero na changamoto zao za muda mrefu ambazo walishindwa kupata ufafanuzi na msaada kwa muda mrefu.
Wanakijiji hao walianza kwa kuomba kujengwa kwa shule ya sekondari katika eneo lililopo shule ya msingi Kurusanga, ambapo wao walisema ndio eneo ambalo lipo jirani zaidi kwa watoto wao tofauti na saivi wanavotembea umbali mrefu kufuata elimu ya sekondari katika shule ya sekondari Salama.
Pia, waliomba watengenezewe barabara katika kijiji chao kwani wamekuwa wakipata shida hasa kipindi cha mvua barabara hawana kabisa. Kero nyingine waliomba kwenye kituo cha Afya Kurusanga waongezwe wahudumu wa kutoa huduma za Afya ili kuwapunguzia mwendo wa kufuata matibabu na vipimo mbali na eneo hilo ambapo inatokana na uchache wa wataalamu katika kituo cha Afya.
Baadhi ya wanakijiji cha Kurusanga wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji katika mkutano wa Kusikiliza kero na changamoto
Ndugu Mbilinyi aliwashukuru wanakijiji hao kwa kutoa na kueleza kero na changamoto wanazokabiliana nazo na aliwaahidi kwenda kuzifanyia kazi ikiwemo suala la kuongeza wataalamu katika kituo cha Afya Kurusanga, na suala la ujenzi wa shule ya sekondari katika eneo la shule ya msingi Kurusanga aliwaambia anaenda kuunda timu ya wataalamu kutoka Halmashauri ambao watakuja kukagua eneo na kupima, na aliwaahidi atakuja kulitolea majibu baada ya taarifa kutoka kwa wataalamu hao itakapo kamilika.
Sula la matengenezo ya barabara ya Kurusanga, aliwaahidi kulifikisha sehemu husika kwani ye hana majibu nalo.
Pia, aliwashauri wanakijiji kuongeza nguvu katika ujenzi wa mabweni katika shule ya sekondari Salama, ili wanafunzi waweze kulala shuleni, huku wakisubiria kibali cha ujenzi wa sekondari mpya pale wataalamu watakaposhauri kulingana na taarifa itakavyoeleza.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda