Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Januari 9,2020 limejadili,kuridhia na kupitisha rasimu ya Bajeti yenye zaidi Bilioni 34ikiwa ni makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka ujao wa fedha 2020/2021 ambapo makusanyo ya ndani ya Halmashauri ni zaidi ya bilioni1.
Akiwasilisha makisio na mpango wa bajeti kwa mwaka 2020/2021 katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Kibara Afisa Mipango kwa niaba ya Mkurugenzi Bi.Julieth Ntuku alisema Halmashauri inatarajia kukusanya kupokea na kutumia zaidi ya bilioni 34 ambapo Kati ya fedha hizo zaidi ya bilioni 22 nifedha kutoka Serikali kuu maalum kwa ajili ya mishahara ya Watumishi, zaidi bilioni 3 zimeelekezwa kwenye miradi ya maendeleo huku zaidi ya bilioni956 kwaajili ya matumizi menginineyo na bilioni 6 maombi maalum kwaajili ya kujenga Jengo la Halmashauri.
Afisa Mipango alitaja Vipaumbele vya bajeti hiyo kwa mwaka wa fedha 2020/2021 kwa kuboresha huduma za afya na lishe katika ngazi ya jamii na Vituo vya huduma za afya kwa kutenga fedha za uratibu,usimamizi na kujenga uwezo wa maswala ya lishe ikiwa ni pamoja na kutenga shillingi 1,000 kwa kila mtoto mwenye umri wa chini ya Miaka mitano kwa ajili ya huduma za lishe, kukamalishaji wa miradi ambayo haikukamilika ikiwemo sekta ya afya na maboma katika Shule ya Msingi na Sekondari,Kuhamasisha kilimo hasa cha alizeti,kuimarisha shughuli za kuinua Uchumi wa wananchi na kuimarisha miundombinu, pamoja na kutenga fedha za kutosha kwaajili ya kulipa mishahara ya Watumishi na kuajiri Watumishi wapya.
"Mhe.Mwenyekiti rasimu hii ya mpango wa Bajeti ya Halmashauri ni makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2020/2021, rasimu hii itaendelwa kujadiliwa na kupatiwa ushauri kwenye vikao vya ngazi ya Mkoa,Ofisi ya Rais TAMISEMI pamoja na Wizara ya Fedha Mipango kabla ya kujadiliwa na kupitisha na Bunge"alisema Bi Ntuku.
Akizungumza wakati wakufunga kikao Kaimu Mwenyekiti ambaye pia ni Diwani wa kata ya Nasimo Mhe.Sabato M.Mafwimbo
amewataka madiwani kutoa ushirikiano kwenye zoezi la ukusanyaji mapato,pamoja na kubaini vyanzo vipya vya mapato iliyasaidie kuharakisha maendeleo kwakuzingatia asilimia 40 ya mapato ya ndani yanatakiwa kuelekezwa kwenye miradi ya maendeleo.
"Mkurugenzi wewe pamoja na timu yako tuendelee kuchapa kazi,tunasifa ya kushirikiana Kati ya timu ya madiwani na watalam u , tuendelee kufanya kazi kwa umoja,uwadilifu na ushirikiano."
Rasimu ya Bajeti 2020/2021 imeandaliwa kwakuzingatia Ilani ya chama tawala(CCM),Mwongozo wa Bajeti mwaka 2020/2021,Mpango wa pili Maendeleo wa Taifa wa Miaka mitano,Malengo ya maendeleo endelevu(SDGs),Dira ya Taifa ya maendeleo ya Taifa 2025,pamoja na mpango Mkakati wa Miaka mitano wa Halmashauri kwa kuzingatia Sheria ya fedha ya serikalin za Mitaa.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda