Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Bunda wametoa malalamiko yao kwa wakala wa barabara vijijini na Mjini (TARURA),kwa kushindwa kutekeleza miradi yao kwa wakati.
Malalamiko hayo yametolewa katika Mkutano wa Baraza la Madiwani robo ya pili mwaka wa fedha 2020/2021 uliofanyika katika ukumbi wa Kanisa la Kibara Aprili 1,2021.
Akizungumza Diwani wa kata ya Kibara Mhe, Mtamwega Mgaywa amesema kuwa Barabara zinzotengenezwa na TARURA hazina viwango bora hali inayopelekea kuharibika ndani ya muda mfupi hivyo kuwa changamoto kubwa kwa watumiaji.
‘Barabara hizi zimekuwa chini ya viwango mvua inaponyesha kidogo tu barabara inakatika’.alisema mhe Mgaywa
Naye, Diwani wa Kata ya Chitengule Mhe. Mkama Brown amemuomba Meneja wa TARURA kutembelea katika vijiji na kuacha kukaa ofisini ili akaone changamoto zinazo wakabili Wananchi.
Kwa upande wake Meneja wa TARURA Mhandisi Kassim Shabani amewaeleza wajumbe kuwa katika mwaka wa fedha 2020/2021 TARURA ina mikataba ya shilingi milioni 886 kwaajili ya ukarabati wa miundombinu ya barabara za mjini na vijijini katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.
‘Tunaishukuru Serikali kwakuendelea kutupatia fedha kwaajili yakurekebisha barabara zenye changamoto’.alisema Mhandisi Shabani
TARURA inaendelea matengenezo ya kawaida katika barabara zenye umbali wa kilometa 2 mpaka7 katika Tarafa ya Kenkombyo ambapo asilimia 50 ya ujenzi unaendelea na Tarafa ya Chamriho kilomenta 10 na asilimia 80 ya ujenzi unaendelea.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda