Katibu Tawala Mkoa wa Mara Bwa. Albert Msovelo amewataka Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda kuishi na Sheria ,taratibu na miongozo ya Utumishi wa Umma.
Hayo amesema Septemba 9, 2021 katika kikao na Watumishi kilichofanyika katika ukumbi wa Kanisa la Kibara.
Bwa. Msovela amesema kuwa Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda waone umuhimu wa kuzingatia kanuni na taratibu za utumishi wa umma ili kila mmoja awajibike katika nafasi yake
‘’kila mtumishi hapa aone umuhimu wa kufuatilia na kuishi na kanuni, taratibu na miongozo ya utumishi wa Umma’’
Bwa. Msovela alisisitiza watumishi kuwa na nidhamu,kila mtumishi aone umuhimu wa mtumishi mwenzake pamoja na kuthamini kazi za mtumishi mwenzake.
‘’Hakuna aliyebora kuliko mwengine nidhamu na heshima ni muhimu kwa kila mtumishi ili kujenga mahusiano mazuri katika kazi’’amesisitiza Bwa Msovela
Aidha Bwa. Msovela alitoa rai kwa Watendaji wa Kata na Vijiji ,Elimu kata na Watumishi wengine wasio wa makao makuu kuhakikisha wanajibika kwa nafasi zao katika vituo vyao vya kazi.
‘kwa watendaji wa kijiji kuhakikisha wanasoma taarifa ya mapato na matumizi,wahudumu wa afya kuhakikisha wanatoa huduma nzuri kwa wagonjwa ili kuepusha malalamiko yasiyo ya lazima’’alisema Bwa. Msovela
Kwa hatua nyingine Bwa.Msovela alisisitiza ukusanyaji wa mapato kwakuhakisha taarifa za mapato zinafika mkoani kila mwezi ikiwa na kuziba mianya ya upotevu wa mapato kiholela.Pamoja na kuhakikisha a asilimia 40 inapelekwa kwa Wanawake,Vijana na Watu wenye ulemavu. Sambamba na kusimamia miradi yote ya Halmashauri.
‘’Niwajibu kuhakikisha mapato yanaongezeka na sio kupungua kwakuhakikisha mianya ya kupoteza mapato haipo tena kuanzia sasa’’amesema Bwa Msovela.
Kwa Upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Bi.Changwa Mkwazu alitoa shukrani kwa katibu Tawala Mkoa kwa kuona umuhimu wakuja kuongea na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda
Aidha Bi. Mkwazu aliahidi kushirikiana na Watumishi wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda katika kufuata kanuni,taratibu na miongozo ya utumishi wa umma.
‘’Ni kuahidi tu Ndugu katibu Tawala Mkoa kuwa maelekezo yote uliyoyatoa mimi kama kiongozi wa hawa watumishi niahidi kwamba yatatekelezwa’’amesema Bi Mkwazu
Naye, Mary Ruseke Afisa Mifugo kwa niaba ya watumishi wengine ametoa shukrani kwa Katibu Tawala Mkoa kwakufika kutoa maelekezo lakini pia kusikiliza kero za watumishi.
‘Sisi kama watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda tumefarijika na ujio huu,tunaamini mabadiliko yatapatikana kuanzia sasa’amesema Bi.Ruseke
Halmashauri ya Wilaya ya Bunda ina jumla ya Kata 19,Tarafa 3 na Vijiji 78 na vitongo 378 pamoja na majimbo mawili Mwibara na Bunda.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda