Kamatiya Fedha, Uongozi na Mipango yaHalmashauri ya Wilaya ya Bunda imefanya ziara ya kutembelea Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri hiyo.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Mhe. SabathoMafwimbo amewataka wananchi kuonesha ushirikiano ili kuhakikisha miradiinakamilika kwa wakati.
Wito huo ameutoa wakati wa ukaguzi wa mradi wa Ukamalishaji wa Jengo la Wazazi naujezi wa Jengo la upasuaji ambao utagharimu kiasi cha shilingi Milioni 200 Katika Kituo Cha Afya Kasuguti. Amesema jengo hilo likikamilikalitakuwa msaada mkubwa kwa wananchi hivyo ni muhimu wanakijiji kuoneshaushirikiano ili mradi ukamilike kwa wakati.
"Nguvu za wananchi nimuhimu Katika kutoa ushirikiano kwa Serikali"
Pia Mhe. Mafwimbo amemuagiza Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Kijiji ambae piani Diwani wa kata ya Kasuguti Mhe. Alex Msege kuwasimamia wananchi ipasavyo ilikuongeza kasi ya ujenzi.
Miradi mingine iliyotembelewa na kamati hiyo ni pamoja na Zahanati ya Kihumbu ambayo ujenzi wake umegharimu kiasi cha shillingi Milioni 109, Milioni 30 zikiwa zimetolewa na wadau wa maendeleo, TANAPA Kama sehemu ya mchango wao Katika Kijiji hicho. Pia kamati ilitembelea kituo cha afya Mugeta ambacho kimetengwa kwa ajili na wagonjwa wa COVID-19.
"Kukamilika kwa zahati ya kihumbu imekua msaada mkubwa hasa kwakina mama na watoto"
Kwa upande wao wananchi wameipongeza serikali kwa kusogeza karibu huduma. Wamesema miradi ya afya ikiwemo zahanati ya Kihumbu imesaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa changamoto ya kusafiri umbali mrefu kufuata huduma katika vijiji jirani
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda