Pamba ni zao la nne linaloingizia Taifa kipato kwa asilimia 99 inalimwa na Wakulima wadogo na asilimia 70 mpaka asilimia 80 huuzwa nje.
Taasisi ya utafiti wa kilimo Tanzania(TARI) kupitia kituo chake cha utafiti Ukiguru kilichopo mkoani Mwanza imetoa mafunzo ya Mradi wa Cotton Victoria kwa maafisa ugani wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda,Butiama,Serengeti na Musoma DC.
Akizungumza katika mafunzo hayo kwa maafisa ugani Bwa.Robert Ngumuo Mtafiti kutoka TARI amesema lengo la mafunzo hayo ni kuweka uelewa wa pamoja yanamna yakumletea kumlima tija ili aweze kunufaika katika zao la pamba pamoja na kuonesha umuhimu wa kufanya utafiti wa zao la pamba ili kuongeza uzalishaji kwa Mkulima.
Kwa muda mrefu zao la pamba limekuwa na teknolojia moja tu katika vipimo vya upandaji wa mbegu,teknolojia ambayo watalamu wanaeleza kuwa imepitwa na wakati.
Bw.Ngumuo ameeleza kuwa teknolojia hiyo ya vipimo iliyokuwa ikitumika katika upandaji wa mbegu ni sentimeta 90 kwa sentimenta 40(mstari na mstari sentimeta 90 pia mbegu na mbegu sentimeta 40).
“Utafiti unaonesha kuwa teknologia ya 90 kwa 40 imetumika kwa muda mrefu lakini bado haijamkomboa mkulima”.alisema Ngumuo utafiti
Ngumuo anasema kuwa teknologia ambazo wanazifanyia utafiti ilikuleta kwa wakulima,zitaweza kuwaomboa wakulima na kupunguza gharama za uzalishaji
Ngumuo anazitaja teknologia hizo mpya ambazo TARI inazifanyia utafiti kuwa ni sentimeta 50 kwa sentimenta 30,(mstari na mstari 50,mbegu na mbegu sentimeta 30),sentimeta 60 kwa 30.
Nyingine ni vipimo vya sentimenta 70 kwa 30 pamoja na sentimeta 80 kwa 30
‘Vipimo hivyo vinaweza kubadilika vikawa sentimenta 50 kwa 16.67,60 kwa 16.67,70 kwa 16.67 pamoja na 80 kwa 16.67.”alisema Ngumuo
Aidha Ngumuo anaeleza kuwa kwenye teknologia zote hizo,lengo lake kubwa ni kuongeza mazao shambani,kwani matumizi ya teknologia ya zamani 90 kwa 40 imekua ikiacha nafasi kubwa kufanya mkulima kutonufaika kutokana na kupata mazao machache.
“teknologia hii inongeza mavuno yanakuwa mengi kwa sababu kunakuwa na miche mingi ya pamba katika eneo dogo”.alisema Ngumuo
Naye, Dkt Paul Saidia Mtafiti kutoka TARI Ukiguru anasema kuwa kuwa teknologia hizo mpya,suala,la mbolea ni muhimu sana kwani uchaguzi mzuri wa mbolea hufanya mazao yakue kwa ustawi mzuri zaidi.
Dkt Saidia anaeleza zaidi kuwa utumiaji wa mbolea za kisasa,ikiwemo urea na mbolea yakukuzia mmea uweze kuwa na afya nzuri na kuzaa matunda ya kutosha.
“Kwa kutumia mbolea kila mche mmoja wa pamba unatakiwa kuwa na vitumba kuanzia 20 na kwenda juu,lakini ukifanya vizuri na kuzingatia kanuni zote mche unaeza kubeba vitunda hadi 40 hata mbolea ya samadi ni sahihi kwa matumizi”. Anasema Dkt Saidia
Benson Mturi Afisa kilimo Halmashauri ya Wilaya ya Bunda alisema amefurahia elimu hiyo iliyotolewa na hivyo itawasaidia kuwafundisha wakulima upandaji mzuri wa mbegu za pamba kwa kuzingatia kanuni na taratibu zinazoelekezwa katika kilimo cha pamba.
“kupitia mafunzo haya yaliyotolewa na TARI naamini sisi ndio tutakuwa mabalozi wazuri kwa Wakulima wetu.”alisema Mturi
Kwa upande wake Bwa. Ruge Kelvin Afisa Kilimo Mkoa wa Mara Ametoa wito kwa Maafisa kilimo wote walioshiriki katka mafunzo haya kuzingatia maelekezo yaliyotolewa pamoja na kuyafanyaia kazi`
“ kila Halmashauri ikawe mfano wa kuigwa kupitia mafunzo haya naomba tusiangushane”Anasema
Bwa. Kelvin amewapongeza na kuwashukuru TARI kwakuendelea kuwa bega kwa bega na Wakulima kwa kuendelea kutoa Elimu ambayo inatija kwa Mkulima.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda