Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Daktari Hamidu Adinani alifungua mafunzo ya siku mbili kwa Wahudumu wa Afya ngazi ya Vijiji yaliyofanyika katika Shule ya Sekondari Mwibara siku ya tarehe 5/10/2023.
Daktari Adinani alisema, lengo la mafunzo haya ni kuwawezesha Wahudumu wa Afya ngazi ya Vijiji kuwatambua watu wenye Lishe duni katika Jamii, ambao inapelekea kupata Utapiamlo na Udumavu kwa Watoto walio chini ya miaka Mitano (5).
“Tunawapa mafunzo haya ili muweze kuwatambua kina Mama Wajawazito, Watoto na Wazee wenye changamoto ya Lishe katika Vijiji na kuwasaidia katika kuwaelimisha namna bora ya kuweza kuandaa chakula chenye mchanganyiko wa Lishe yenye virutubisho sahihi kwa kufuata makundi muhimu ya vyakula ili kuepusha kupata Utapiamlo na Udumavu kwa Watoto.” Alisema Daktari Adinani.
Kaimu Mganga Mkuu aliwaagiza kwenda kufanya kazi kwa bidii kwa kushirikiana na Wataalamu waliopo katika Zahanati pamoja na Hospitali zilizopo katika Kata na Vijiji, ili kumuhaisha mtu mwenye changamoto ya Utapiamlo mara tu watakapomtambua mapema.
Alisema ili kuondokana na zana potofu za imani za Kishirikina katika Vijiji na Kata zetu mnatakiwa mkawaelimishe kwenda kwenye vituo vya Afya mara tu wanapoona mtu ana changamoto za Lishe duni. Kwa kumshauri kwenda kwenye vituo vya Afya kwaajili ya kuonana na Wataalamu.
Pia aliwaomba kutoa ushirikiano kwa kina Mama Wajawazito kwa kuwashauri na kuwaelimisha umuhimu wa kuhudhuria Kliniki mara tu wanapojihisi kuwa ni Wajawazito na sio kusubiria hadi miezi mitatu ndio aanze kuhudhuria Kliniki, hii itaepusha kupata madhara wakati wa kujifungua na wakati mwingine kuepusha vifo vya Mama na Mtoto maana watashauriwa vyema na Wataalamu waliopo katika vituo vya Afya jinsi ya kuandaa Lishe iliyo bora hadi atakapojifungua salama.
Daktari Adinani alisema, mmekuwa msaada mkubwa sana kwenye sekta hii ya Afya kwa ngazi ya Vijiji, ni matarajio makubwa kwa Halmashauri ya Wilaya kwamba, baada ya mafunzo haya mtaenda kuyafanyia kazi kwa kushirikiana vyema na Wataalamu waliopo katika Zahanati na Hospitali zetu huko katika Kata na Vijiji kwa kuwatambua mapema wale wote wenye viashiria vya hatari kwa kuhakikisha mnawawahisha katika vituo vya Afya mapema.
Naye, Mkufunzi wa mafunzo hayo ambaye ni Afisa Lishe wa Mkoa wa Mara Bw. Benson Sanga alisema lengo la mafunzo haya ni kutambua majukumu yenu katika Vijiji kwa kuhakikisha mnafuatilia matibabu ya Utapiamlo mara tu mnapohisi mtu amepata changamoto kwa kuhakikisha anafika katika kituo cha Afya mapema na kupatiwa matibabu.
Pia walifundishwa, namna ya kupima hali ya Lishe kwa Watoto wote kuanzia umri wa miezi 6 hadi miaka 5 ili kuweza kutambua hali ya udumavu kwa Mtoto ambaye amekosa Lishe iliyo bora.
Pia walifundisha namna ya kutoa elimu kwa Mama Mjamzito kwa kuhakikisha anahudhuria Kliniki mapema na kwa wakati kwa kula Lishe iliyokamili kwa kufuata makundi sahihi katika kuandaa Lishe.
Mafunzo hayo yalihudhuriwa na Wahudumu wa Afya ngazi ya Vijiji 96 kutoka katika Vijiji 48 na Kata 12 za Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda