Halmashauri ya Wilaya ya Bunda kushirikiana na wadau wa Elimu PCI na Project Zawadi wametoa motisha kwa Walimu wa Kuu wa shule zilizopata matokeo mazuri ya Darasa la nne na Darasa la Saba.
Akizungumza katika hafla ya utoaji tuzo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Bunda Bwa.Nico Kayange 2020, amesema lengo la tuzo hizi ni mkakati wa kujenga hamasa na kuwavuta mioyo Walimu iliwaendelee kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi,"kwa ninyi walimu ambao hamjapata zawadi kupitia hafla hii naomba mpate hamasa yakufanya vizuri zaidi ili mwaka mwengine mpate"Alimpongeza Afisa Elimu Msingi kwakuja na wazo la kutoa hamasa kwa Walimu ili waendele kufaya vizuri zaidi.
Bwa.kayange alitoa rai kwa walimu kuwa na nidhamu ya kimavazi ,tabia na pia kuwepo na ushirikiano katika majuku yao na mbali na majukumu yao.Alitoa shukurani za kipee kwa wadau wa elimu na kuwapongeza walimu wa Shule zilifanya vizuri"Azima yetu tuwe wa kwanza lakini pia tunakemeana mahala ambapo hatujafanya vizuri na hatuwezi kuwa kimya kwa hiki tulichokipata tunayo sababu ya kupongezana"
Naye,mgeni rasmi kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa Bwa Elisongo Mshiu alisema tukio hili la kihistoria na kipekee,niwapongeze walimu kwakuendelea kujituma kwa bidii na ufanisi,"sisi tunatekeleza Ilani ya chama" kwa walimu ambao hamjafanya kazi vizuri msikate tamaa jitahidini mfanye vizuri.alisema Bwa.Mshiu.Aliendelea kusema Serikali haijawasahau wanafunzi wenye uhitaji Maalum bado inatuma vifaa vya kujifunzia bado serikali inafuatilia wanafunzi wenye uhitaji maalum .alitoa agizo kwa walimu kuhakikisha wanafunzi wanapata chakula wakati wakiwa Shule"walimu mtoe hamasa kwa wazazi pamoja na ushirikiano kuhakikisha wanafunzi wanapata chakula shuleni"
Aidha Afisa Elimu Msingi bwa.Reginald Richard aliwataka walimu kuendelea kutekeleza majuku yao kiufanisi pamoja na kufuata taratibu za ufundishaji ili kuweza kupata matokeo mazuri zaidi. Tunashuku serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mh.Dkt John Pombe Magufuli kwakuweza kupunguza changamoto sekta ya elimu, Tunashukuru wadau wetu wa ELimu PCI na Zawadi Project.]Alisema Bwa Rirchard
Kwa upande wa Meneja Mradi PCI Bi.Juliana Dyegura Alisema binadamu yeyote katika kufanya kazi anapenda kupata motisha,katika elimu Kuna motisha hasi na motisha chanya ambazo kazi yake kubadilisha tabia na kukuza tabia"sisi Kama shirika lengo letu kukuza umahili wakusoma,kuandika na kuhesabu"tunaposimama hapa leo kusema Wilaya yetu ya Bunda imefanya vizuri tunashukuru mungu”.Tunapenda kuwapongeza wote waliofanya vizuri,lakini kwa wenzetu ambao hamjafanya vizuri tuendelee kukazana ili tufike mbali zaidi.
Naye,Mwalimu Mwanaidi Zacharia alitoa shukurani za dhati kwa ofisi ya Mkurugenzi na wadau kwa ujumla,"sisi Kama walimu tumefarijika kwa kilichofanyika siku ya leo inatupa hamasa kujituma zaidi."
Halmashauri ya Wilaya ya Bunda ina jumla ya tarafa tatu,chamriho,kenkombya na Nanaimo,kata 19 na Shule za Msingi 104 Kati ya hizo shule 100 ni za serikali,Shule 3zinamilikiwa na watu binafsi na shule1 ina milikiwa na kanisa la wasabato.hali ya ufaulu wa Darasa la nne ulipanda kutoka asilimia 87 mpaka asalimia 90 kwa mwaka 2019.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda