Halmashauri ya Wilaya ya Bunda imetoa motisha kwa walimu,wanafunzi pamoja na shule zilizofanya vizuri katika Nyanja mbalimbali kwa mwaka 2020.Ambapo tunzo hizo zilijikita katika utunzaji mazingira,Taaluma, uendeshaji wa miradi pamoja na madarasa yanayongea.
Akizunguza katika hafla ya utoaji tuzo iliyofanyika katika ukumbi wa kanisa la Kibara Februari 18,2021 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Bunda Bwa. Amos Kusaja alisema Idara ya Elimu msingi ni idara inayoongea,katika idara zangu zote za halmashauri ya Wilaya ya Bunda elimu msingi inafanya kazi.
“Nampongeza Afisa Elimu Msingi pamoja na timu mzima kwakuendelea kuifanya halmashauri ya wilaya bunda kung’aa kimkoa kwakushika nafasi ya tatu”.alisema Bwa. Kusaja
Aidha Bwa Kusaja ameeleza kuwa bajeti ya 2020/2021 imetengwa milioni mia moja kutoka mapato ya ndani kwaajili ya ujenzi wa madarasa shule za msingi.
Kwa hatua ingine Bwa Kusaja alitoa shukrani kwa Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Dkt John Pombe Magufuli kwakuendelea kupunguza changamoto katika Elimu , wadau wa elimu PCI kwa kuendelea kutoa mafunzo kwa walimu wa KKK,Project Zawadi na NMB bank kwakuendele kuchangia katika ujenzi wa madarasa
“Niwashukuru NMB bank kwasababu wametuahidi kutuunga mkono na mwaka huu wametuhadi watatupa shilingi milioni 10 kwaajili ya ujenzi wa madarasa’.alisema Kusaja
Naye Mgeni rasmi Mkuu wa wilaya Bunda Mhe Lydia Bupilipili alisema katika elimu motisha ni kitu kizuri
“Binadamu yeyote katika kufanya kazi anapenda kupata motisha’.alisema mhe Bupilipili
Aidha Bupilipili amewataka walimu kuongeza juhudi katika kutekeleza majukumu yao kwani hiyo ni moja ya nguzo ya kuimarisha ufaulu katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.
‘panapo kuwa na kwanza na mwisho yupo ninaimani kwa juhudi hizi ufaulu utaongezeka zaidi’.alisema Bupilipili
Mhe Bupilipili aliongeza kusema kuwa kila mmoja ana wajibu wakufanya kazi, na tuongeze juhudi sababu inawezekana kabisa kushika nafasi ya kwanza kimkoa.
Kwa hatua inginge mhe Bupilipili ametowa wito kwa wananchi kuendelea kuwaheshimu walimu ili kuendelea kuleta ushirikiano bora baina ya mwalimu na mwanafunzi.
“Wapo baadhi ya wananchi anapoana Mwanafunzi akiadhibiwa wao wanahukumu mwalimu,waache hiyo tabia mara moja’.alisema Bupilipili
Kwa pande wake Afisa Elimu msingi Bwa. Reginald Richard ametaja mikakati ya idara ya elimu msingi ni kupandisha ufaulu wa darasa la nne kuwa ni 100% na darasa la saba ni 95% kwani dalili za kufikia malengo haya yamewezekana,kudhibiti utoro kwa walimu na wanafunzi,kumaliza tatizo la KKK na kuboresha kamati za maendeleo ya elimu kata.
Bwa. Richard aliwataka walimu kuendelea kutekeleza majukumu yao kiufanisi pamoja na fuata taratibu za ufundishaji ili kuweza kupata matokeo mazuri zaidi.
‘Ushirikiano baina yetu ndio utatufanya tusonge mbele zaidi”alisema Bwa. Richard
Aidha Bw. Richard ametoa shukrani kwa Serikali ya awamu ya Tano kwakuendelea kumaliza changamoto mbalimbali katika elimu na kutengeneza mazingira bora ya kufundisha na kujifunza.
‘kwakweli mpaka tunaishukuru serikali maana mazingira ya shule zetu yanavutia kwa asilimia kubwa’
Naye ,Mwalimu Malindi Majige kutoka shule ya Msingi Mwibara alitoa shukrani kwa niaba ya walimu wengine alitoa shukrani za dhati kwa Serikali ya awamu ya tano kwakuendelea kuangalia masilahi yao pamoja na wadau wengine.
‘sisi kama walimu tunafarijika na tunapata hamasa yakufanya vizuri zaidi’.
Halmashauri ya Wilaya ya Bunda ina jumla ya Tarafa tatu ambazo ni Chamriho,Kenkobyo na Nansimo, ina jumala ya kata 19 na Shule za msingi 104 kati ya hizo shule 100 ni za serikali na 3 na watu binafsi na 1 inamilikiwa na kanisa.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda