Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe Adam Malima Kigoma amepongeza Halmashauri ya Wilaya ya Bunda kwa Kupata HATI SAFI.Katika ukaguzi wa Hesabu za Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019.
Ametoa pongezi hizo katika kikao maalumu cha Baraza la Madiwani kujadili hoja za Ukaguzi kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri kilichoongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe, Sabatho Mafwimbo na Katibu ambaye Kaimu Mkurugenzi Bwa. Stephen Ochieng na kuhudhuriwa na Kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya na Katibu Tawala wa Mkoa Bi.Karolina Mtapula pamoja na wataalamu wa ofisi yake.
Bwa.Ochieng ameliambia baraza la madiwani hali ya hoja zilizopo Halmashauri ya Wilaya ya Bunda kufikia Mwezi juni 2019 ilikua na jumla ya hoja 73 za miaka ya nyuma na 36 za mwaka 2018/2019.Katika hoja hizo 73 za miaka ya nyuma,33 zimejibiwa na kufungwa,4zimpitwa na wakati,17zimjirudia na 14 utkelezaji wake bado unaendelea.’’Katika Mwaka wa fedha 2018/2019 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda imepata HATI SAFI’.Alisema Bwa.Ochieng
Naye Katibu Tawala Mkoa Bi Karolina Mtapula amewataka watendaji wa halmashauri kuongeza ushirikiano na Mkaguzi wa ndani ilikuepuka hoja nyingi,sambamba na hilo kuhakikisha nyaraka zinazohitajika wakati wa ukaguzi ziwasilishwe kwa haraka.
‘Kila Mkuu wa Idara na vitengo mwenye hoja awajibike katika kujibu hoja kwa wakati ili eneo lny shida tulifanyi kazi”.alisisitiza Mtapula
Aidha Mhe.Malima ameitaka Halmashauri kuongeza nguvu zaidi katika ukusanyaji wa mapato ya ndani na kuhakikisha asilimia 40 zinazotakiwa kwenda katika mandeleo zipelekwe kwa wakati kwani ni takwa la kisheria.sambamba na hilo kubainisha kiasi cha fedha zilizopo katika POS Sita zilizopotea pamoja na wahusika warudishe fedha hizo kabla Juni 30,2020.
Malima aliongeza kwa kusema kuwa halmashauri ihakikishe kuwa Hati za maeneo na Majengo wanayomiliki yabainishwe kabla ya kufikia Juni 30,2020.
Mwisho Malima aliagiza Halmashuri kushirikiana na Ofisi ya RAS kuhakikisha Malipa ya Madiwani yanakamilika kabla ya kufikia Juni30,2020 naelekeza kuwa uhakiki ufanyike ili kuweza kukamilisha madai yao.
Makamu Mwenykiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda na Diwani wa kata ya Nansimo Mhe.Sabatho Mafwimbo aliwasisitiza Watumishi wa Halmashauri kuwa ni Watu ambao Serikali imewatuma kuwasaidia wananchi wa Bunda wahakikishe halmashauri isonge mbele katika kuongeza mapato.Amewapongeza kwa namna kila diwani alivoshiriki katika baraza hilo na kuonesha ukomavu katika kujenga hoja kwa maslahi ya wananchi wa Bunda.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda