Halmashauri ya Wilaya ya Bunda imeendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kwakuweka mikakati ili kuwapatia huduma wale wote waishio na virusi vya Ukimwi na kudhibiti maambukizi mapya.
Hayo yamesemwa na Kaimu mratibu wa shughuli za Ukimwi Dkt Damian Makila wakati wa ghafla ya siku ya Ukimwi duniani iliyofanyika katika Kata ya Nyamuswa kijiji cha Nyamuswa.
Dkt.Makila amesema kuwa hali halisi ya virusi vya ukimwi katika Halmashauri ya wilaya ya Bunda ni asilimia 3.8 waliopima virusi vya ukimwi kuanzia Julai hadi Septemba,2020 ni watu 16497 kati ya hao waliogundulika kuishi na virusi vya ukimwi ni Laki moja na elfu sabini na sita.
Dkt makila aliongeza kusema kuwa katika kipindi cha Septemba hadi Julai jumla ya wamegundulika wanavirusi vya ukimwi.
Kwa upande wa mgeni rasmi ambae ni Mbunge wa jimbo la Bunda Mhe Boniface Mwita Getere amewaasa wananchi kuichukulia siku hii kwaajili ya kuwakumbusha jinsi ya kujikinga na maambukizi na virusi vya ukimwi nasio kusheherekea nakufanya mambo yanayoweza kuwa chanzo cha ukimwi huku akiwasisitiza kupima afya zao mara kwa mara.
“Leo ni siku ya ukimwi Duniani na ukiwa na ukimwi usiogope kupima wala kusema”alisema Mhe Getere
Pia Mhe Getere ametoa wito kwa wazazi kuacha tabia yakuwatumia watoto wao wa kike kama njia ya kupata kipato badala yake watoe elimu kwao namna yakujikinga na ukimwi.
“Wazazi na walezi ni ninyi ndio walimu wazuri kwa binti zenu wafundisheni namna yakujikinga na ugonjwa huu”.alisisitiza mhe Getere.
Aidha Maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani yalienda sambamba na uhamasishaji wa kampeni wa upimaji VVU,Tohara kwa vijana wa kiume kuanzia umri wa miaka 10 na kuendelea pamoja na upimaji wa saratani ya shingo kwakina mama.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda