Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Feb 24,2021 limejadili,kuridhia na kupitisha rasimu ya Bajeti yenye zaidi Bilioni 34.5ikiwa ni makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka ujao wa fedha 2021/2022 ambapo makusanyo ya ndani ya Halmashauri ni zaidi ya bilioni1.
Akiwasilisha makisio na mpango wa bajeti kwa mwaka 2021/2022 Afisa mipango Bwa. Dickson Balige kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji alisema Halmashauri inatarajia kukusanya na kutumia zaidi ya bilioni 34.5 ambapo kati ya fedha kiasi cha shilingi bilioni 32 kutoka serikali kuu.
Aidha Balige alisema bajeti ya mapato ya ndani imeongezeka kw sh.71,327,400 kutoka bajeti ya 1,426,548,000 hadi shilingi 1,497,875,400 kwa mwaka wa fedha 2021/2022 sawa na ongezeko la asilimia 4.7 ongezeko hili limetokana na kuimarika kwa mfumo wa ukusanyaji wa mapato.
Balige alitaja vipaumbele vya bajeti hiyo kwa mwaka 2021/2022 kuwa ni kuchangia miradi ya maendeleo,ujenzi wa miundombinu ya shule,kutoa mikopo kwa Wanawake,Vijana na watu wenye ulemavu,kusimamia nakuimarisha ukusanyaji mapato na kuhamasisha ufugaji bora nakutoa chanjo ya mifugo.
“Mhe Mwenyekiti rasimu hii ya mpango wa bajeti ya halmashauri ni makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2021/2022,rasimu hii itaendelea kujadiliwa na kupatiwa ushauri kwenye vikao vya ngazi ya Mkoa,Ofisi ya Rais TAMISEMI pamoja na Wizara fedha Mipango kabla ya kujadiliwa na kupitisha na Bunge’'alisema Balige.
Akizungumza wakati wa kufunga kikao Mwenyekiti wa Halmshauri mhe.Charles Manumbu ambae pia ni Diwani wa kata ya Iramba,alisema ni zoezi la ukusanyaji mapato linahitaji ushirikiano kati ya wataalamu na madiwani pamoja ili kuongeza mapato pamoja na kubaini vyanzo vipya vya mapato.
“Mkurugenzi na timu yako tuendelee kuchapa kazi,tunasifa ya kushirikiana kati ya timu ya madiwani na wataalam ili tusonge mbele na kuifanya Halmashauri kuwa imara’.Aliseme Manumbu
Bajeti ya Halmashauri imeongezeka kwa shilingi 6,886,822,164 sawa na asilimia 20.07.Ongezeko hili linatoka na tarajio la ajira mpya pamojan na matarajio ya watumishi kupanda madaraja.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda