Halmashauri ya Wilaya ya Bunda imeadhimisha siku ya wazee Duniani iliyombatana na kauli mbiu isemayo “Familia na jamii tuwajibike kuwatunza Wazee”.
Maadhimisho hayo yamefanyika leo katika Kijiji cha Nansimo Kata ya Nansimo yakiambatana na ugawaji wa kadi 593 za msamaha wa matibabu ikiwa kadi 323 ni kata ya Nansimo na 270 kata ya Chitengule , ipamoja na utoaji wa huduma za Afya kama vile upimaji,ushauri,Dawa na Rufaa.
Akizungumza mgeni rasmi kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji Bwa.Oscar Jeremia amesema kuwa Serikali inatambua mchango wa Wazee hasa katika kuleta maendeleo ya Taifa letu hivyo katika kuadhimisha siku hii ni moja wapo ya kuthamini mchango wenu.
“wazee mmefanya kazi kubwa sana ndio maana serikali inawaenzi”.
Katika Kuadhimisha Siku ya Wazee,Bw.Jeremiah amesema ipo mikakati madhubuti imeandaliwa na Halmashuri ili kuhakikisha haki za Wazee zinapatikana kwa wakati.
Ameitaja mikakati hiyo kuwa ni kuunganisha wazee wasiojiweza na Mfuko wa TASAF na Afya ya Jamii iliyoboreshwa(CHF),kuwatembelea Wazee na kufanya Mikutano ili kuwasikiliza , kuunganisha na vikundi ili kupata mkopo ya 2% ya Halmashauri,kupinga na kuzuia kiwango kikubwa cha mauaji ya Wazee kwa tuhuma za uchawi ,kuwatambuana na kuhakikisha wazee wote wenye umri wa miaka 60 na kuendelea wanapata vitambulisho vya msamaha wa matibabu.
Aidha Bw.Jeremiah alitoa wito kwa familia na Jamii kuendelea kutunza Wazee ili wasipate upweke.
“Tusiwakimbie wazee maana wao ndo wametukuza mpaka tulipofika”.alisisitiza Jeremiah
Naye Afisa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri Bi Fausta Parali amesema tunapoadhimisha siku ya wazee sio tunakutana tu bali tunapata nafasi yakutambua changamoto mbalinbali zinazowakabili wazee.
Bi. Parali amesema pia kuwa Halmashauri kupitia kitengo cha Ustawi wa Jamii inashughulikia kuwaunganisha wazee na family zao wanapotelekezwa au kutupiwa mzigo wa wajukuu.
“Kila mzee anae achiwa wajukuu na ikiwa wazazi wa mtoto yupo inabidi apatiwe huduma na mzazi wa mtoto huyo”alisisitiza Parali
Katika hatua nyingine muwakilishi wa Wazee Bwa.Asaf Mkama ameishukuru serikali ya awamu ya Tano kwakuendelea kuwa tunza na kuthamini mchango wao.
“Nimefarijika kuona viongozi wetu wanatukutanisha wazee kama sisi kutoa mawazo yetu
Aidha Bwa. Mkama ameiomba serikali kuwapatia miradi mbalimbali kama mashine ya kusaga unga ili waweze kujikomboa kiuchumi na kukidhi mahitaji.
“Tunaomba serikali itupatie miradi itakayo tusaidia kuinua kipato”alisema Mzee Mkama.
Maadhimisho hayo yameambatana na uzinduzi wa Mabaraza ya Wazee ya Kata ya Chitengule na Nansimo ikiwa jumla ya Wazee 9,994 wametambuliwa katika vijiji 78 na ka Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda