Hayo yamesemwa na Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Bi.Beatrice Gwamagobe Machi 8, 2021 katika kilele cha maadhiisho ya siku ya wanawake yaliyofanyika katika Kata ya Chiterngule kijiji cha Busambara kwa kauli mbiu“Mwanamke katika Uongozi chachu kufikia Dunia yenye Usawa’‘.
Aidha Gwamagobe alisema kuwa Halmashauri kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii imeendelea kutoa asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa kutoa mkopo kwa Watu wenye ulemavu 2 Vijana 4 na Wanawake asilimia 4 ambapo mikopo hiyo imeweza kuinua kipato cha Wanawake wengi pamoja na makundi mengine yanayonufaika na mkopo usio na riba.
‘uwepo wa mkopo usio na riba umeweweza kusaidia wanawake wengi kwa kuendeleza shughuli za kijasiliamari na kupelekea vikundi hivyo kufanikiwa’’alisema Gwamagobe
NayeMgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mhe Lydia Bupilipili amewaasa wanawake kujisimamia kupitia fedha za mikopo wanazopatiwa ili kukuza vipato vyao na familia kwa kujihusisha na shughuli ndogondogo za jamii kama ufugaji,kilimo na kuacha kumtegemea mwanaaume pekeake .
‘kila mwanamke atambue kuwa siku ya wanawake imewekwa kwaajili ya kukumbushwa majukumu ya wanawake wote katika jamii’’.alisema Bupilipili
Mhe Bupilipili alitoa wito kwa familia zinazoendelea kumgandamiza mwanamke kiukatili kuwacha mara moja,kwani kuendelea kufanya hivo ni kumrudisha nyumaMwanamke.
‘lazime unyanyasaji na ukatili kwa Mwanamke ufike mwisho’alisema Bupilipili
Kwa upande wa Wanawake waliohudhuria maadhimisho hayo wamesema kuwa watafanyia kazi yale yote walioelekezwa na Mkuu wa Wilaya na kuwa mstari wa mbele kupinga na kupambana na ukatili katika jamii zao na kuhimiza wanawake wengine kufanya kazi.
Kwa hatua ingine Gwamagobe alisema kuwa licha ya juhudi zinazofanywa na serikali bado wanawake wanakabiliwa na changamoto za ufukiaji wa huduma za jamii kama elimu,Afya na upatikanaji wa huduma za maji kwa ukaribu,ambapo kuna baadhi ya vijiji wanafuata maji umbali mrefu.
Maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani hufanyika kila mwaka Machi 8, ambapo huambatana na shughuli mbalimbali mpaka kufikia kilele. Kwa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda kupitia Idara ya maendeleo ya jamii Watumishi wanawake walitembelea kituo cha Watoto wanaoishi mazingira magumu kilichopo Bunere,Kupanda miti katika hospitali ya Wilaya pamoja na kutoa semina kwa Wanafunzi wa kike katika shule ya Sekondari Mwibara
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda