Hali ya ufaulu wa mtihani wa kidato cha 2 pili mwaka 2020 imeongezeka kwa asilimia 6 kutoka asilimia 83 kwa mwaka 2019 hadi kufikia asilimia 89 kwa mwaka 2020.
Hayo yamesemwa na afisa taaluma wilaya ya Bunda Januari Izumba, wakati akisoma taarifa ya tathimini ya ufaulu wa mitihani ya taifa mwaka 2018,2019,2020. Ambapo alisema kuwa licha ya kukutana na changamoto mbali mbali katika ufundishaji Halmashauri imefanikiwa kuimarisha ubora wa elimu na kusababisha kupungua kwa wanafunzi wanaopata daraja 0 licha ya ufaulu huo kupanda kwa asilimia chache.
Nae mkuu wa wilaya a ya Bunda Lydia Bupilipili ambae alikuwa mgeni rasmi amewaasa Walimu kupenda kazi zao na kuacha kusingizia changamoto maaana kila kazi inachangamoto zake,hivyo wahakikishe wanafanyia kazi na kufanikisha jitihada zote ambazo zimewekwa kwa ajili ya kuongeza ufaulu mashuleni.
Aidha Mhe Bupilipili alisema kuwa walimu wanatakiwa kushirikiana na kuwapenda watoto mashuleni maana baadhi ya watoto wanatoka katika familia ambazo hazina uelewa juu ya elimu na hazitoi ushirikiao ili wanafunzi wasome katika mazingira mazuri, hivyo walimu hawana budi kuwafundisha kwa utaratibu mzuri ambao utasaidia kuongeza ufaulu.
‘ Wanaowajibu wa kutekeleza kila hitaji la wanafunzi kwa kila hali ili kuongeza ufaulu’.alisema Bupilipili
Licha ya mafanikio na mabadiriko hayo izumba aLIsema kuwa kunachangamoto zinazoikabili idara ya elimu sekondari ikiwemo upungufu wa walimu hasa masomo ya sayansi,upungufu wa vifaa vya kujifunzia mashuleni, utoro kwa wanafunzi ambao wamekuwa wakihusishwa katika shughuli za kijamii.
Halmashauri ya Wilaya ina Tarafa tatu Chamriho,Kenkyombio na Nasimo pamoja na shule za Sekondari 17 zinazomilikiwa naSerikali na 2 zinamilikiwa na binafsi.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda