Mapambano dhidi ya umasikini katika nchi yetu yalianza takribani miaka sitini iliyopita mara tu baada ya uhuru.
‘kama mnakumbuka baba wa Taifa Mwl.Julis Nyerere aliwataja maadui watatu wa Taifa hili ni umasikini,Maradhi na Ujinga lakini ukiweza kupambana na adui mmoja ambae ni umasikini unakuwa katika nafasi nzuri ya kupamba na maadui wawili ambao ni maradhi pamoja na ujinga’’
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mhe Joshua Nassari wakati wa ufunguzi wa Kikao kazi cha kujenga uelewa kuhusu sehemu ya pili ya awamu ya tatu ya TASAF Agosti 10,2021 katika Ukumbi wa Halmashauri uliopo Bunda Mji.
Mhe. Nassari amesema kuwa Elimu kwa walengwa inabidi itolewe kila wakati na wawezeshaji ili kuwawezesha walengwa kutumia vizuri fedha wanazopata pamoja na miradi wanayoanzisha ili kujikwamua katika umasikini.
‘’Wawezeshaji mtapimwa kwakuangalia mafanikio ya walengwa, Tutapima kwamba kwa namna gani mmefanya kazi hii kwakuangalia mafanikio gani yanapatikana na lengo lililowekwa na Serikali katika mpango wa pili wa TASAF ’’alisema Mhe Nassari
Mhe Nassari ametoa wito kwa waheshimiwa madiwani kuwa mabalozi katika maeneo yao pamoja nakuelekeza wananchi madhumuni halisi ya mpango wa TASAF kipindi cha pili katika kuwahikikisha Wananchi wanatoka katika hali duni na kujikwamua katika umasikini i.
‘mafunzo haya yamelenga kwenu viongozi ili kuitambua maana halisi ya mpango huu bila kuyumbishwa na matakwa ya kisiasa,kiundugu na urafiki ambao mmeujengea katika jamii zenu,mkatusaidie kuwa mabalozi ili mpango huu uwe na tija’’alisema Mhe.Nassari
Awali akisoma hotuba kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha kujenga uelewa kuhusu seheumu ya pili ya awamu ya TASAF mtaalamu kutoka makao makuu Bwa.Elius Muyomba amesema tathimini ya utekelezaji wa kipindi cha kwanza cha awamu ya tatu imeonyesha kwamba program hii imechangia katika kufikiwa kwa azma serikali ya kupunguza umasikini nchini.
‘Takwimu zinaonesha kwamba umasikini wa mahitaji ya msingi kwa kaya za walengwa umepungua kwa asilimia 10 na umasikini uliokithiri kwa kaya za walengwa umepungua kwa asilimia 12 hii ni kutokana na walengwa kujikita katika shughuli za kukuza kipato zikiwemo ufugaji,kilimo,uvuvi na kufanya miradi ya ujasiriamali’Alisema Bwa.Muyomba
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Bwa.Kilemba Irobi ametoa shukrani kwa Serikali kwakuendelea kuweka mkakati bora kwa walengwa ili kuwahikikisha wanajikwamua katika umasikini.
‘’kwa utaratibu huu wakuanzisha vikundi na uwepo wa miradi hii itasaidia kukuza kipato cha walengwa’
Aidha Mhe Irobi ameto rai kwa wananchi kuendelea kusimamia miradi na fedha wanazopata kwani TASAF haitakuwepo siku zote.
‘’ Walengwa wakumbuke kuwa TASAF haitakuwepo siku zote hivyo wajiwekee akiba kwa kufanya shughuli za kujipatia kipato’’alisema Mhe Irobi
TASAF kipindi cha pili Awamu ya Tatu kinatekelezwa kwa Halmashauri zote 184 za Tanzania Bara na Wilaya zote za Zanzibar na kwa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda inatarajia kufanya zoezi hili katika Vijiji 22 ambapo hapo awali havikufikiwa .
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda