Halmashauri ya Wilaya ya Bunda imepokea jumla ya msaada wa madawati 200 kutoka bank ya NMB tawi la Bunda siku ya tarehe 7/2/2025, ambapo meneja wa bank Kanda ya Ziwa, pamoja na timu nzima ya bank tawi la Bunda walikabidhi madawati hayo kwa uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda mgeni rasmi akiwa ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Bunda Ndugu Salum Mtelela, kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Bunda.
Akikabidhi msaada huo, meneja wa bank ya NMB Kanda ya Ziwa, Bi. Faraja Ng'ingo alimshukuru katibu Tawala kwa kuweza kushiriki katika zoezi la upokeaji wa madawati,pia aliupongeza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda pamoja na wananchi kutoka Mwiruruma, Mumagunga na Buguma kwa kushiriki katika mapokezi hayo.
Bi.Ng'ingo alisema, tunayofuraha kuona mnashirikiana nasi katika mambo mbalimbali hususani ya kijamii, hapa, sisi ni wenyeji sasa na zaidi tunafurahia kuona wenyeji wetu kutambulika na kushirikishwa katika masuala mbalimbali ya kuchangia katika sekta ya elimu kwa ujumla na ushirikiano huu ndio unaotufanya kuwa bank kinara katika kujali na kujihusisha na masuala mbalimbali ya jamii hapa nchini.
“Tunatambua juhudi za serikali ya Awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluh Hassan ya kusimamia upatikanaji wa huduma Bora za elimu, kwa nguvu zote na kwa kuboresha mazingira ya elimu mjini na vijijini, hatunabudi sisi bank ya NMB kuendelea kuipongeza serikali na kuunga juhudi katika kuboresha sekta ya elimu." Alisema
Pamoja, na juhudi kubwa zinazofanywa na serikali sisi kama wadau wa Maendeleo tutaendelea kuunga mkono juhudi hizi za maendeleo kwa kuisaidia jamii, kwani jamii hizi ndizo zinazosaidia bank ya NMB kuwa hapa ilipo.
" Leo hii tunakabidhi madawati haya 200 kwa mgawanyo wa shule tatu za msingi ambazo ni Mumagunga, madawati 50, Buguma madawati, 50 na Mwiruruma madawati 100 yote yakiwa na thamani ya Tshs Million 20." Alisema
Tunawashukuru kwa kutambua kuwa bank ya NMB ni mahala salama pa kukimbilia, hii inaonyesha jinsi mnavyothamini mchango wetu kwenu katika kuchangia Maendeleo katika sekta ya elimu kwa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda