Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Bw. George S. Mbilinyi kwa kushirikiana na wakuu wa Idara na vitengo, wamefanya ziara ya kukagua na kutembelea miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri siku ya tarehe 2/1/2025 kwa lengo la kutazama maendeleo ya utekelezaji wa miradi, kupokea maoni ya uboreshaji wa miradi na kupokea changamoto za uendeshaji wa miradi na kuzitolea utatuzi.
Katika ziara hiyo, walitembelea na kukagua miradi kumi(10)ambayo ni Shule ya msingi Namibu A, Shule ya Sekondari Mahyolo,ujenzi wa Zahanati ya Nyamitwebili, Sekondari ya Kasuguti, Zahanati ya Mwiseni, Shule ya Sekondari ya wasichana Mara, Shule ya Sekondari Muranda, kituo cha afya Isanju, Shule ya msingi Igundu, Shule ya msingi Bulomba pamoja na Shule ya Sekondari ya Amali Makwa.
Aidha, baada ya ziara hiyo Bw. Mbilinyi amewahimiza wakuu wa Idara na vitengo kufanya ufuatiliaji wa mara kwa mara ili kuhakikisha miradi yote inakamilika kwa wakati sahihi.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda