Halmashauri ya Wilaya ya Bunda ilianzishwa rasmi 1/7/2016 baada ya kugawanywa kwa Halmashauri ya awali ya Wilaya ya Bunda. Halmashauri hii ni moja kati ya Mamlaka Tisa za Serikali za Mitaa zilizopo katika Mkoa wa Mara.
Karibu 80% ya Wakazi wanaoishi katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda hutegemea kilimo katika kuendesha maisha yao. Ardhi inayofaa kwa kilimo ni kilomita za mraba 164,622 hekta. Eneo linalotumika kwa kilimo ni hekta 122,931.
Mazao Makuu ya chakula yanayolimwa ni Mahindi, Mtama, Mihogo, na Viazi Vitamu.
Mazao Makuu ya biashara ni Pamba, Alizeti na Dengu.
KARIBUNI KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA BUNDA!!!!!
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0754335739
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda